Yanayojiri

Afcon Qualifier 2021:Kundi A: Namibia, Mali, Guinea, Chad. Kundi B: Uganda, Sudan Kusini, Malawi, Burkina Faso. Kundi C: Sudan, Ghana, Afrika Kusini, Sao Tome na Principe. Kundi D: Gambia, Gabon, DR Congo, Angola. Kundi E: Morocco, Mauritania, Jamhuri ya Kati, Burundi. Kundi F: Rwanda, Msumbiji, Cape Verde, Cameroon (mwenyeji). Kundi G: Togo, Kenya, Misri, Comoros. Kundi H: Zimbabwe, Zambia, Botswana, Algeria (Watetezi). Kundi I: Senegal, Guinea-Bissau, eSwatini (zamani Swaziland), Congo Brazzaville. Kundi J: Tunisia, Tanzania, Libya, Equatorial Guinea. Kundi K: Niger, Madagascar, Ivory Coast, Ethiopia. Kundi L: Sierra Leone, Nigeria, Lesotho, Benin.Afcon Qualifier 2021:Jumatano, Novemba 13, 2019. Namibia v Chad, Burkina Faso v Uganda, Malawi v Sudan Kusini, Sudan v Sao Tome na Principe, Angola v Gambia, Jamhuri ya Kati v Burundi, Cameroon v Cape Verde, Senegal v Congo Brazaville, Guinea-Bissau v E-eSwatini, Nigeria v Benin, Sierra Leone v Lesotho.. Afcon Qualifier 2021:Alhamisi, Novemba 14, 2019. Mali v Guinea, Ghana v Afrika Kusini, DR Congo, Msumbiji v Rwanda, Misri v Kenya, Togo v Comoros, Algeria v Zambia.Afcon Qualifier 2021:Ijumaa, Novemba 15, 2019. Morocco v Mauritania, Zimbabwe v Botswana, Tunisia v Libya, Tanzania v Equatorial Guinea.Afcon Qualifier 2021:Jumamosi, Novemba 16, 2019. Ivory Coast v Niger, Madagascar v Ethiopia.Afcon Qualifier 2021:Jumapili, Novemba 17, 2019. Guinea v Namibia, Chad v Mali, Uganda v Malawi, Sudan Kusini v Burkina Faso, Afrika Kusini v Sudan. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

MTG United ndiyo mabingwa wa kombe la vijana Afrika Mashariki.

Na Anthony Aroshee

Jumatano Julai 1, 2015

Timu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 16 ya MTG United ya kutoka kaunti ya Kilifi nchini Kenya, imetwaa kombe la ubingwa wa mashindano ya vijana wa Afrika Mashariki yaliyofanyika Moshi nchini Tanzania.

MTG United ilishindwa katika fainali ya mashindano ya mwaka 2012.

 

Kikosi cha MTG United cha mwaka huu kilichosheheni vijana wenye umri wa chini zaidi ya miaka 16, kiliwashinda wenyeji wao timu ya Buguruni Youth ya Tanzania kwa njia ya mikwaju ya matuta huku mlinda mlango wa MTG United Zainabu Mwalimu akiokoa matuta mawili.

MTG United ilitinga fainali baada ya kuwashinda wenyeji CHRISC Tanga katika mchezo wa nusu fainali.

Licha na kunyanyua ubingwa huo, mchezaji wa MTG United Salama Ali ambaye alifunga mabao matano katika michuano hiyo ya Afrika Mashariki, alipata tuzo ya mwanasoka bora kwa upande wa wasichana katika kitengo cha vijana wenye umri wa chini ya miaka 16.

Wasichana wa MTG wamekuwa wakishiriki kwenye mashindano hayo ya Afrika Mashariki tangu mwaka 2009.

Mashindano hayo ya kombe la Afrika Mashariki ni michezo ya vijana, elimu na utamaduni kwa wasichana na wavulana wenye umri wa chini kati ya miaka 11 na 16 na uandaliwa kila mwaka huko Moshi nchini Tanzania.

Zaidi ya vijana 2000 kutoka Afrika Mashariki walishiriki kwenye michuano ya mwaka huu.

Katika matokeo ya mechi za makundi:

MTG United (2 – 0, 3 – 0) Moshi Local 2

MTG United(2 – 0, 0 – 1) Sport for Real Change  

 

Chapa Barua pepe

Share

Powered by OrdaSoft!

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin