Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

Tononoka Sekondari yajiandaa kwa mashindano ya mkoa nchini Kenya.

 

Na Anthony Aroshee

Jumanne Julai 7, 2015

Mabingwa wa Soka kwa shule za upili za wavulana katika kaunti ya Mombasa nchini Kenya, wamefanya mazoezi yao ya mwisho asubuhi ya siku ya jumanne Julai 7, 2015 kwenye uwanja wa Bomani kwa maandalizi ya kushiriki kwenye mashindano ya jimbo la pwani nchini humo.  

Shule hiyo ya Tononoka Secondary, chini ya kocha mkuu Salato Omar ambaye zamani alikuwa mwanafunzi na nahodha wa shule hiyo, wanaiwakilisha kaunti ya Mombasa kutokana na kuwa ni vijogoo baada ya kuwashindna Likoni Secondary mabao 2-1 katika mchezo wa fainali.

Likoni Secondary pia watawakilisha Kaunti ya Mombasa kwenye mashindano hayo kutokana na kuwa, Kaunti ya Mombasa ni mabingwa watetezi katika Soka. Timu hizo zitaondoka asubuhi ya siku ya jumatano Julai 8 kuelekea mjini Voi. 

Mashindano ya jimbo la pwani yataandaliwa kuanzia alhamisi Julai 9 hadi jumamosi Julai 11 kwenye mji wa Voi katika kaunti ya Taita Taveta huku ile ya kitaifa, ikifanyika kwenye Kaunti ya Machakos kuanzia Julai 28 mwaka huu.

 

Chapa Barua pepe

Share

Powered by OrdaSoft!

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin