Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

Kinyanganyiro cha michuano ya Soka ya Taifa Ngano Super Cup inaanza rasmi Mombasa nchini Kenya.

 

Na Anthony Aroshee

Ijumaa Julai 31, 2015

Michuano ya kabumbu ya makala ya 11 kuwania taji la Taifa Ngano Super Cup katika Kaunti ya Mombasa Pwani ya taifa la Kenya, inaanza rasmi siku ya ijumaa Julai 31, 2015 kwenye uwanja wa Mombasa Sports Club(MSC).

Mtanange wa kufungua dimba ni mpambano wa kundi A baina ya Green Eagles na Nyota FC ya kutoka mtaa wa Magongo wilayani Changamwe. 

Mwandalizi wa michuano hiyo inayoandaliwa kila mwaka, Mohammed Madigi, ameidhibitishia Dawatilamichezo.com kuwa, mshikemshike huo utashirikisha jumla ya vilabu 16 vilivyogaanywa katika makundi manne ya timu nne kila kundi.

Washindi wawili kutoka katika kila kundi kati ya makundi hayo manne, watafuzu robo fainali huku michuano hiyo ikikamilika siku ya jumapili ya Septemba 13, 2015 kwa mchezo wa fainali. Mechi za hatua ya makundi zitapigwa kwenye uwanja wa Mombasa Sports Club huku baadhi ya  mitanange ya mkumbo wa mtoano, ikigaragazwa katika uwanja wa Mombasa Sports Mbaraki.

Mabingwa watetezi wa mashindano hayo ni klabu ya Mombasa Maize Millers ambao waliwashinda Bodo Glut FC mabao 2-1 katika patashika ya fainali ya mwaka jana 2014.

Bingwa wa michuano hiyo ya Taifa Ngano ya mwaka huu 2015, atapokea kitita cha shilingi 100,000 pamoja na seti moja ya jezi na taji la Taifa Ngano Super Cup. Mshinde wa pili atakabidhiwa burungutu la shilingi 50,000 pamoja na seti moja ya jezi na taji la Taifa Ngano Super Cup la mshinde wa pili. 

Timu zitakazotinga fainali, licha na zawadi hizo za fedha watakazopata, pia watapokea bandali za unga wa mahindi.

Mashindano hayo yanafadhiliwa na kampuni ya kutengeneza uga wa mahindi ya Mombasa Maize Millers Limited ambayo imetumia jina la kampuni yake tanzu ya Taifa Ngano kwa kima cha shilingi 600,000 kwa fedha za Kenya.

Makundi Kamili:

Kundi A

Green Eagles

Nyota FC

Fetuwe

ESC Youth

Kundi B

Gulshan Youth 

Congo Kids

Mlandege

Mombasa Sports Club

Kundi C

Mombasa Maize Millers

Bibla

Nyundo FC

Action Boys

Kundi D

Bodo Glut

Talanta

Wanderers

Malindi United

Chapa Barua pepe

Share

Powered by OrdaSoft!

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin