Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

Amani FC, Birikani FC zashinda katika mechi za ligi ya FKF Kinango nchini Kenya.

 

Na Anthony Aroshee

Ijumaa Septemba, 2015

Shirikisho la Kandanda nchini Kenya FKF kwenye tawi dogo la Kinango katika Kaunti ya Kwale nchini Kenya, liliandaa ligi ya mechi za mtoano za shirikisho hilo zilizopepetwa kwenye viwanja mbali mbali katika eneo hilo.

Timu ya Amani FC walifuzu hadi hatua nyengine kwa kuwatandika Fulugani United FC mabao 2-0 kwenye uwanja wa shule ya msingi ya Fulugani kwenye eneo la wodi ya Kasemeni huku mabao hayo yakivurumishwa kimiani na Mwadiga Ndegwa pamoja na Dalmas Dalu.

Rising Star walitangulia kufunga bao kupitia Musa Kibwana katika dakika ya 60 kabla ya Amani FC kusawazisha bao hilo lililofungwa na Ali Ngao kunako dakika ya 80.

Nayo timu ya Birikani FC pia ilisonga mbele baada ya kuwazaba Bofu United mabao 3-0 yaliyopachikwa wavuni na Mwamunga Munga aliyefunga bao la kwanza katika dakika ya 19 kabla ya kufunga bao la tatu na la ushindi kunako dakika ya 75.

Tobias Mramba alipachika wavuni bao la pili dakika ya 60.

Mazeras United FC pia walifuzu kwa jumla ya mabao 5-3 dhidi ya timu ya Mwamdudu FC huku Mazeras United ikishinda michezo mitatu nayo Mwamdudu FC wakipoteza mechi mbili katika mitanange tano waliokutana kati yao. Ligi hiyo ya FKF Kinango katika kaunti ya Kwale, inaandaliwa na Mwanaloma Kitumdo.

 

Chapa Barua pepe

Share

Powered by OrdaSoft!

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin