Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

Njuguna Joseph ni kipa mwenye ujasiri langoni.

 

Na Francis Mudzo

Jumatano Januari 6, 2016

Ni golikipa wa kupigiwa mfano na anayekuja kwa kasi ya kutisha kwenye eneo la kaunti ndogo ya Mwihoko katika kaunti ya Kiambu nchini Kenya huyu sio mwengine ila Njuguna Joseph mwenye umri wa miaka 15 anayetoa huduma zake kwa kituo cha kukuza soka ya vijana ya Changes Soccer Academy.

Njuguna alianza kusakata soka inayotengezwa kwa makaratasi kama ilivyo desturi ya maeneo ya mashinani akiwa mchezaji wa ndani lakini siku zilivyoendelea aligundua kwamba, sehemu inayomfaa uwanjani ni golini. Hali hiyo ilimpelekea Njuguna kujitambua na kuanza kujifunza kuwa mlinda lango alipokuwa akicheza na watoto wenzake kwenye mchezo wa Tufe.

Kufikia mwaka jana 2015 baada ya timu ya Changes Soccer Academy kuanzishwa na kina dada wawili Angela Nabwire na mwenzake Mildred Cheche, Njuguni alipata fursa kwenye timu hiyo. Ni ambayo kufikia sasa ndio imetimiza miezi kumi lakini imefanya mambo mengi katika kaunti ya Kiambu nchini humo kwa kukuza vipawa vya vijana waliokuwa wamepotelea mitaani.

Ni miaka ya awali, Njuguna alianza kucheza akiwa katika darasa la sita kwenye shule ya msingi ya Ndiini iliyoko mjini Ruiru akiwa katika shule hiyo ya msingi, ndiye aliyekuwa golikipa wa kutegemewa. Baada ya kukamilisha masomo yake katika shule hiyo alijiunga na shule ya upili ya St.Peter's Embu ambako ni kiungo muhimu kiwanjani.

Njuguna ana matumaini ya kuchezea timu kubwa katika nchi za ugaibuni, kwani alitaja mchezaji kama mlinda mlango wa timu ya taifa ya Uhispania na zamani Real Madrid Iker Casilas ambaye sasa hivi anaidakia FC Porto ya Ureno kuwa, kichocheo chake katika soka katika nchi za nje.

Licha ya kuvutiwa na kuchochewa na wachezaji wa nje, hajawasahau wachezaji wa nyumbani wanao mtia moyo wa kuendelea kutimiza ndoto yake, ni kama vila mlinda mlango wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars na klabu ya Lillestrøm ya nchini Norway, Anorld Origi. Akizungumza na Dawatilamichezo.com, Njuguna alisema kuwa ana maono ya kufika mbali katika  maisha yake ya soka.

“Nimeona dalili njema za kwenda mbali kutokana na wakufunzi wangu wanao nifunza kugundua uwezo wangu wa ulinda lango hivyo nitafuata kanuni na sheria wanayo niambia ili nitimize ndoto yangu”, Njuguna alifafanua.

Njuguna alisema hayo wakiwa kwenye ziara ya kimichezo katika kaunti ya Mombasa waliko cheza na timu kadhaa ikiwemo timu ya Chaani Youth. Mmoja wa mkufunzi wake Mildred Cheche alisema kuwa kipa huyo ana weledi mkubwa wa kulinda eneo lake licha ya umri alionao.

“Amekuwa akiokoa timu sana hasa inapofika awamu ya mikwaju ya matuta yeye hujituma vilivyo kuona kwamba anabeba timu yake na wachezaji wenzake”, kocha Cheche aliidokezea Dawatilamichezo.com.

 

Chapa Barua pepe

Share

Powered by OrdaSoft!

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin