Simona Halep bingwa wa Wimbledon Open amshinda Serena Williams fainali

Imeandikwa .

Na Dawati La Michezo

Jumamosi, Julai 13, 2018

Simona Halep kutoka Romania ndiye bingwa mpya wa Michuano ya Wimbledon Open 2019 katika mchezo wa mpira wa Tenisi upande wa Wanawake baada ya kumshangaza mkongwe Mmarekani Serena Williams kwa kumshinda seti 2-0 za 6-2, 6-2 katika fainali iliyofanyika jijini London Uingereza Jumamosi hii ya Julai 13, 2019..

Mwanadada huyo, mwenye umri wa miaka 27, alimshinda Williams ambaye ni bingwa mara saba wa michuano hiyo ya Wimbledon Open na pia ni ushindi wake wa kwanza kupata dhidi ya mchezaji mkongwe katika fainali ya mashindano ya Wimbledon Open.

Hilo ni taji lake la kwanza kwa Halep kushinda katika Mashindano hayo ya Wimbledon Open likiwa ni taji lake la pili la Grand Slam. Mromania huyo pia ni bingwa wa taji la michuano ya French Open, aliloshinda mwaka jana 2018.

Halep, ambaye zamani aliorodheshwa wa kwanza kwa ubora duniani katika mchezo huo, alimshinda Williams mwenye umri wa miaka 37, ambaye ni bingwa mara 23 wa mataji makubwa ya Grand Slam.

Mmarekani huyo amewai kumshinda Halep mara tisa katika mechi 10 walizokutana hapo awali.

Williams ametinga kwa mara ya 13 mfululizo katika fainali ya michuano mikubwa ya Grand Slam huku akipoteza kwa Mjerumani Angelique Kerber seti 2-0 za 6-3 6-3 katika fainali ya mwaka jana 2018. Kerber alishindwa na Mmarekani huyo kwenye fainali ya mwaka 2016.

Taji lake la mwisho la Grand Slam Williams kushinda ilikuwa ni la Australian Open mwaka 2017, kabla ya kuamua kupumzika kwa muda wa mwaka mmoja kwenda kujifungua mtoto wake, Alexis Olympia.

 

Chapa