Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

Michuano ya French Open kuanza bila ya Serena Williams na Roger Federer

 

Na Victor Abuso

Jumapili, Mei 28, 2017

Makala ya 116 ya michuano ya Tennis ya French Open yanaanza kutifua vumbi Jumapili hii katika uwanja wa Roland Garros jijini Paris.

Bingwa mtetezi wa michuano ya Australian Open wa upande wa wanawake Mmarekani Serena Williams na bingwa mtetezi wa upande wa wanaume Roger Federer kutoka Uswizi hatawashiriki katika michuano hii.

Serena Williams hatakuwepo kwa sababu ni mjamzito.

Hata hivyo, mabingwa watetezi wa michuano hii kwa upande wa wanaume Novak Djokovic kutoka Serbia na Garbine Muguruza kutoka Uhispania watakuwepo kutetea mataji yao.

Wachezaji wa kiume 32 akiwemo Andy Murray, Novak Djokovich, Stan Wawrinka, Rafael Nadal watapambana katika hatua mbalimbali za mwondoano huku Angelique Kerber, Karolina Pliskova, Simona Halep, Slina Svitolina wakiwa ni miongoni mwa wanawake 32 watakaotoana kijasho katika michuano hii itakayomalizika tarehe 11 mwezi Juni.

 

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin