Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

Bondia wa uzani mzito Deontay Wilder akamatwa na bangi

 

Na Dawati La Michezo

Jumanne, Juni 20, 2017

Bingwa wa ndondi za uzani mzito duniani anayeshikilia taji la WBC Deontay Wilder ameshtakiwa kwa kumiliki bangi.

Maafisa wa polisi katika eneo la Tuscaloosa jimbo la Alabama wamesema kuwa alikamatwa alipokuwa akipeleka gari lenye vioo linalomficha aliye ndani yake kutoonekana.

Maafisa wanasema kuwa walipata dawa hiyo ndani ya gari lake.

Wakili wa Wilder Paul Patterson aliambia kitengo cha habari cha Tuscaloosa kwamba dawa iliopatikana ndani ya gari hilo haikuwa yake na kwamba mtu mwengine alitumia gari hilo wakati bondia huyo alipokuwa safarini.

Aliambia chombo hicho kwamba Deontay amekuwa safarini kwa siku kadhaa.

Alirudi nyumbani leo kutoka Georgia akiwa anaendesha gari lake la Rolls Royce na kuchukua gari jingine aina ya Cadillac Escalade kutembea maeneo mbalimbali ya jimbo hilo.

Wilder alishtakiwa na polisi na kuachiliwa huru kwa dhamana ya dola 1000.

Maafisa walipata ruhusa ya kulisaka gari hilo kabla ya kufanikiwa kupata kiwango cha bangi kutoka kwa gari hilo, taarifa ya maafisa wa polisi wa Tuscaloosa ilisema.

Pigano la mwisho la Wilder lilikuwa la ushindi wa raundi ya tano kwa njia ya Knockout dhidi ya Gerlad Washington alipotetea taji lake la WBC ambalo amemiliki tangu 2015.

                                                                                                                                                                                                  Kwani Hisani Ya BBC

 

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin