Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

Mkondo wa 5 Ligi Kuu ya Ndondi nchini Kenya unaanza Alhamisi hii Mombasa

Na Charles Charonga

Alhamisi, Novemba 09, 2017

Mapigano ya mkondo wa tano na wa mwisho wa Ligi Kuu katika mchezo wa ndondi nchini Kenya yanaanza Alhamisi hii Novemba 09 kwenye uwanja wa Mbuzi ulioko Kongowea eneo bunge la Nyali katika kaunti ya Mombasa na kukamilika Jumamosi ijayo Novemba 11.

Hii ni baada ya mapigano ya mkondo wa nne wa ligi hiyo nchini humo kukamilika wiki iliyopita kwenye ukumbi wa Madison Square Garden katika kaunti ya Nakuru.

Mapigano ya Mombasa yatakuwa ni fursa nzuri ya kubaini mbichi na mbivu baina ya klabu ya Majeshi (DEFABA) na mabingwa watetezi wa ligi hiyo Kenya Polisi maarufu kama ‘Chafua Chafua’.

Klabu ya Polisi, inayojivunia mabondia wengi katika timu ya taifa chini ya mwamba wa zamani wa timu ya taifa ‘Hit Squad’ kocha George ‘Forman’ Onyango, italazimika kutumia kila mbinu katika mapigano hayo ya mkondo wa tano ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kuhifadhi taji lao.

Klabu ya Magereza ambayo miaka ya nyuma ilivuma katika mashindano ya ligi kuu nchini, inatarajiwa kutoa upinzani mkali kwa Polisi na Majeshi katika mapigano hayo ya mkondo wa tano huku klabu ya mseto ya Pwani, iliyomaliza mapigano ya mjini Nakuru kwa alama mbili pekee, ikitarajiwa kukaza buti zaidi kutokana na kwamba itakuwa ikizichapa mbele ya mashabiki wake wa nyumbani.

Katika mapigano ya mkondo wa nne wa ligi kuu yaliyoandaliwa mjini Nakuru, mabingwa wa zamani wa ligi hiyo klabu ya Majeshi (DEFABA) iliibuka mshindi kwa alama 25 mbele ya mabingwa watetezi Kenya Polisi iliyokuwa ya pili baada ya kuambulia alama 19.

Klabu ya Magereza inayofunzwa na kocha wa timu ya taifa Patrick Maina iliridhika katika nafasi ya tatu kwa alama 5 ikifuatwa na klabu ya Soweto iliyojikusanyia alama nne katika nafasi ya 4.

Klabu za Dallas na Kentrack zote za Nairobi ziliandikisha alama tatu kila mmoja katika nafasi ya 5 na 6 mtawalia huku Klabu ya Pwani, Kenyatta National Hospital KNH, Nairobi na Oksa zikipata alama mbili kila mmoja. Kongowea kutoka Mombasa ilipata alama moja pekee huku Kibra, Nakuru, Thika, Ndenderu na Kisumu zikiondoka patupu bila alama yeyote katika mapigano hayo.

Endapo klabu ya Majeshi itashikilia uzi huo huo wa ushindi dhidi ya wapinzani wao wakuu ‘Chafua Chafua’ basi itakuwa ni zawadi nzuri kwa aliyekuwa naibu mkufunzi Collins ‘Fitti’ Bulinda aliyeuwawa na majambazi jijini Nairobi wiki mbili zilizopita.

Baadhi ya klabu zinazotarajiwa pia kutoa upinzani katika mapigano hayo ni Soweto ya Nairobi iliyomaliza mapigano ya mkondo wanne katika nafasi ya nne kwa alama nne, Dallas(zamani Kenya Railways), Kentrack, Kenyatta National Hospital KNH na Oksa inayofunzwa na Omar Kassongo aliyekuwa bingwa wa Afrika katika uzito wa heavy.

Klabu nyingine zinazotarajiwa kushiriki katika masumbwi hayo ni Ndenderu ya kocha wa zamani wa timu ya taifa ‘ Hit Squad’ Peter Mwarangu, Kibra, Nakuru Amateur ya kocha Mwangi ‘Carlos’ Muthee, Kisumu United ya Lawrence ‘Cobra’ Jaoko, Thika, Kongowea na Nairobi.

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin