Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

Mombasa West yanyanyua taji la NG-CDF Changamwe kwa wanaume Mombasa Kenya 

 

Na Mohammed Mwaruwa

Alhamisi, Julai 20, 2017

Klabu ya Mombasa West ilishinda taji la NG-CDF Changamwe katika kaunti ya Mombasa nchini Kenya kwenye mchezo wa mpira wa wavu (Voliboli) upande wa wanaume.

Mombasa West walinyanyua Ubingwa huo baada ya kuitandika klabu ya Changamwe seti 3-0 kwenye mchezo wa fainali kabla ya kuichabanga klabu ya Ashton seti 3-0 katika mechi ya nusu fainali na kufuzu fainali. Katika mechi ya hatua ya robo fainali, Mombasa West waliwakung’uta Mikadini seti 3-0.

Kabla ya kutinga fainali, klabu ya Changamwe iliishinda klabu ya Refinery Neighbours seti 3-2 katika mechi ya nusu fainali kabla ya kuicharaza klabu ya Tumaini seti 3-0 kwenye mchezo war obo fainali. Port Reitz waliwatoa Sea Side kwa kuwazaba seti tatu kwa bila.

Kuhusu matokeo mengine ya hatua ya robo fainali, Refinery Neighbours waliwachapa New Flat seti 3-0, Ashton waliwatandika Tumaini seti 3-0 huku Changamwe wakiwalaza Port Reitz seti 2-0.  

Na katika matokeo ya mechi za hatua ya makundi, katika kundi A, Mombasa West ilizishinda klabu za New Flat na Mega seti 3-0 mtawalia huku New Flat ikiizaba Mega seti 3-0.  Katika kundi B Ashton ilipata ushindi wa seti 3-0 dhidi ya Port Reitz na St.Charles Lwanga mtawalia huku Port Reitz ikiichapa mara mbili St.Charles Lwanga seti 3-1 mtawalia.

Kundi C, Refinery Neighbours waliwafunga Mikadini na Changamwe seti 3-0 mtawalia, Changamwe waliwacharaza Bokole na Tumaini seti 3-0 katika kundi D.

 

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin