Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

Changamwe Ladies bingwa wa taji la NG-CDF Changamwe katika mchezo wa Voliboli nchini Kenya

 

Na Mohammed Mwaruwa

Alhamisi, Julai 20, 2017

Klabu ya Changamwe Ladies ndio vinara wa mashindano ya kuwania taji la NG-CDF Changamwe katika kaunti ya Mombasa nchini Kenya kwenye mchezo wa mpira wa wavu (Voliboli) baada ya kuizaba klabu ya Bomu Ladies seti 3-0 katika fainal upande wa wanawake.

Changamwe Ladies walitinga fainali kwa kuifunga klabu ya Refinery Neighbours seti 3-2 nayo Bomu Ladies walifuzu fainali kutokana na ushindi wa seti 3-0 dhidi ya timu ya Port Reitz katika mechi za nusu fainali.

Na katika mechi za hatua ya robo fainali, Refinery Neighbours waliwatandika Mikadini seti 3-0 nao Bomu Ladies pia wakaandikisha matokeo kama hayo dhidi ya klabu ya Ashton.

Kuhusu matokeo ya mechi za hatua ya makundi, katika kundi A, Refinery Neighbours waliandikisha matokeo mazuri dhidi ya Bomu Ladies na Tumaini ya seti 3-2 na seti 3-0 mtawalia. Nayo Bomu Ladies waliwafunga Tumaini seti 3-0 huku klabu ya Changamwe wakiwashinda Port Reitz na Airport seti 3-0 kila mmoja katika kundi B.

Kwenye kundi C, Ashton waliwafunga Mikadini seti 3-2 kabla ya kuwalaza Sea Side seti 3-0 wakati klabu ya Mikadini pia wakipata matokeo kama hayo ya seti 3-0 dhidi ya timu ya Sea Side.

Mashindano hayo yaliyofanyika kwenye viwanja vya Changamwe, yalishirikisha jumla ya timu 21, 9 za wasichana na nyingine 12 za wanaume. 

 

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin