Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

Timu ya taifa ya wanawake ya mchezo wa magongo nchini Marekani yasema inabaguliwa

 

Na Dawati La Michezo

Jumanne, Machi 28, 2017

Maseneta 14 nchini Marekani wameiandikia barua Shirikisho la mchezo wa mpira wa magongo wa kuteleza barafuni nchini humo kushughulikia kwa haraka malalamishi yanayoikumba timu ya taifa ya wanawake.

Timu ya taifa ya wanawake inadai kuwa inaonewa kuhusu malipo ya marupurupu yao. Wachezaji hao wanadai kubaguliwa na kulipwa mshahara mdogo ikilinganishwa na wenzao wa kiume.

Wanasisitiza kuwa ikiwa malalamishi yao hayatatekelezwa, watasusia mashindano ya dunia yanayoanza siku ya Ijumaa nchini humo.

Maseneta wamesema wameshtushwa na taarifa kuwa Shirikisho la mchezo huo linatumia Dola Milioni 3.5 kuimarisha mchezo huo lakini wachezaji wa kike wanabaguliwa.

Ripoti zimekuwa zikisema kuwa timu ya wanaume nao imetishia kususia mashindano ya dunia yatakayofanyika nchini Ufaransa mwezi Mei ikiwa matakwa ya wenzao hayatatekelezwa.

 

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin