Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

Caster Semenya awasilisha rufaa nyingine katika mahakama ya Uswis

Na Emmanuel Makundi 

Jumapili, Juni 2, 2019

Bingwa wa mbizo za mita 800 raia wa Afrika Kusini, Caster Semenya amewasilisha rufaa nyingine katika mahakama kuu ya Uswisi, akipinga kushindwa katika kesi ya kuamua kuhusu kiwango cha homoni mwilini mwake.

Mahakama ya kimataifa ya michezo, CAS ilitupilia mbali rufaa ya Afrika Kusini iliyokuwa inapinga sheria mpya za shirikisho la riadha duniani IAAF, zinazotaka wakimbiaji wa kike wenye homoni zaidi zipunguzwe.

Semenya mwenyewe amesema "mimi ni mwanamke na mwanamichezo mahiri, IAAF haitanizuia jinsi nilivyo," alisema mwanariadha huyo.

Taarifa iliyotolewa Jumatano ya wiki hii inasema kuwa Semenya ataiomba mahakama ya Uswis itupilie mbali uamuzi wa Cas na kuongeza kuwa kiini cha rufaa yake ni haki ya msingi ya binadamu.

Wakili Dorothee Schramm ambaye ataongoza rufaa ya Semenya, amesema sheria za IAAF zinakiuka sheria za wazi kabisa za msingi za sera ya Uswisi.

Kwa sheria za sasa, Casater Semenya na wanariadha wengine wa kike ambao homoni zao zimezidi kiwango, watahitajika kutumia dawa maalumu ili kuzipunguza waweze kushindana katika mbio za kuanzia mita 400.

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin