Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

Mwanariadha Mkenya Jemima Sumgong apatikana na kosa la kutumia dawa iliyopigwa marufuku

 

Na Dawati La Michezo

Jumamosi, Aprili 8, 2017

Jemima Sumgong, mwanariadha wa Kenya wa mbio ndefu aliyeshinda medali ya dhahabu katika mbio za Marathon kwa upande wa wanawake wakati wa Michezo ya Olimpiki mwaka 2016 nchini Brazil amebainika kuwa alitumia dawa ya kumwongezea nguvu mwilini.

Sumgong mwenye umri wa miaka 32 na bingwa wa mbio za London Marathon, amebainika kuwa alitumia dawa iliyopigwa marufuku baada uchunguzi uliofanywa na Shirikisho la mchezo wa riadha duniani IAAF.

Hili ni pigo kwa mwanariadha huyu ambaye hivi karibuni alikuwa ametangaza kuwa atakwenda jijini London tarehe 23 mwezi Aprili kutetea taji lake la London Marathon aliloshinda mwaka uliopita.

Hata hivyo, kumekuwa na uhaba wa maelezo kuhusu uchunguzi huu uliofanywa na IAAF licha ya ripoti za awali kuonyesha kuwa mwanariadha huyo alikuwa safi na hakuwahi kutumia dawa za kuongeza nguvu mwilini.

Sumgong alikuwa mwanamke wa kwanza kuishindia Kenya medali ya dhahabu katika mbio za Marathon.

 

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin