Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

Paul Lonyangata na mkewe Purity watawala mbio za Paris Marathon

 

Na Dawati La Michezo

Jumanne, Aprili 11, 2017

Wanariadha kutoka nchini Kenya Paul Lonyangata na mkewe Purity Rionoripo ndio mabingwa wa makala ya 41 ya Paris Marathon yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita nchini Ufaransa.

Lonyangata alimaliza mbio za Kilomita 42 kwa muda wa saa mbili, dakika sita na sekunde 10, akifuatwa na Mkenya mwenzake Stephen Chebogut, aliyemaliza katika nafasi ya pili kwa muda wa saa 2, dakika 6 na sekunde 56.

Mkenya mwingine Solomon Yego, alimaliza katika nafasi ya tatu kwa muda wa saa mbili, dakika saba na sekunde 13.

Rionoripo naye alishinda mbio hizo kwa muda wa dakika saa 2, dakika 20 na sekunde 55 na kuweka rekodi mpya kwa upande wa wanawake.

Huu ni ushindi wa kihistoria kwa mume na mke kushinda mashindano haya.

Huu ni ushindi mkubwa kwa wakenya baada ya kupokea habari mbaya kutoka kwa Chama cha riadha duniani IAAF, kuwa bingwa wa olimpiki katika mbio hizi mwaka 2016 Jemima Sumgong alitumia dawa iliyopigwa marufuku ya kuongeza nguvu mwilini.

Mbali na taji la Olimpiki, Sumgong alikuwa anatetea taji la London Marathon ambalo sasa hatakwenda kushiriki tarehe 23 mwezi huu wa Aprili baada ya kubainika kutumia dawa hiyo.

Hata hivyo, IAAF inasubiriwa kutoa ripoti zaidi kuhusu uchunguzi huu.

 

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin