Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

Mashindano ya Ubingwa wa Taekwondo yafanyika Kilifi nchini Kenya.

 

Na Anthony Aroshee

Jumatano Julai 29, 2015

Mashindano ya wazi ya makala ya 4 ya ubingwa wa mchezo wa Taekwondo katika Kaunti ya Kilifi eneo la Pwani ya nchi ya Kenya, yaliandaliwa kwenye ukumbi wa shule ya Pwani Secondary Vocational School for the deaf mwishoni mwa wiki iliyopita.

Vilabu 10 vya wasichana na wavulana vikiwemo vya watu wakubwa, vijana na watoto vilishiriki kwenye mashindano hayo ya siku moja.

Klabu za watu wazima zilipangwa katika kitengo cha watu wakubwa zilikuwa ni Kilifi Township, The Legends, Kilifi Taekwondo, Chumani, Majaoni, Takaungu, Mapimo Polytechnic na klabu ya Mtopanga ya kutoka Kaunti ya Mombasa, iliyoshiriki kama timu mwaalikwa.

Katika kitengo cha vijana wenyewe umri wa kati ya miaka 15 na 17, timu zilikuwa ni Kilifi Taekwondo, Roka, Magarini na shule ya msingi ya Majaoni wakati timu hizo hizo ndizo zilizoorodheshwa tena  kwenye kitengo cha watoto wenye umri wa chini ya miaka 14.

Mashindano hayo yalifadhiliwa na afisa mkuu katika idara ya kilimo, ustawi wa mifugo na uvuvi katika serikali ya Kaunti ya Kilifi, Baha Nguma ambaye zamani alikuwa mwanataekwondo.

 

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin