Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

Klabu ya Kilifi Taekwondo kidedea katika mchezo wa Taekwondo nchini Kenya.

 

Na Anthony Aroshee

Alhamisi Julai 30, 2015

Klabu ya Kilifi Taekwondo ni mabingwa wa jumla katika mashindano ya wazi ya makala ya 4 kuwania ubingwa wa mchezo wa Taekwondo katika Kaunti ya Kilifi nchini Kenya.

Kilifi Taekwondo walikuwa kidedea baada ya kujikusanyia nishani tano za dhahabu tatu za fedha na moja ya shaba huku klabu ya Majaoni ikichukua nafasi ya pili kwa kupata nishani moja ya dhahabu tano za fedha na nne za shaba.

Katika kitengo cha watu wakubwa, wenye umri wa zaidi ya miaka 18, klabu ya Kilifi Taekwondo pia ndiyo iliyomaliza katika nafasi ya kwanza wakifuatiwa na timu ya Mtopanga ya kutoka Kaunti ya Mombasa waliokuwa wa pili. Klabu ya The Legends ilikuwa ya tatu.

Klabu ya Roka, ilikuwa ya kwanza kwenye kitengo cha vijana wenye umri wa kati ya miaka 15 na 17 huku klabu ya Magarini ikichukua nafasi ya pili. Klabu ya Kilifi Taekwondo ilikuwa ya tatu.

Kulikuwa pia na mashindano ya watoto wenye umri wa chini ya miaka 14 ambapo klabu ya Kilifi Taekwondo iliongoza ikifuatiwa na klabu ya Majaoni katika nafasi ya pili huku timu ya Roka, ikiridhika kwenye nafasi ya tatu.

Michuano hiyo ilifadhiliwa na afisa mkuu katika idara ya kilimo, ustawi wa mifugo na uvuvi katika serikali ya Kaunti ya Kilifi, Baha Nguma ambaye zamani alikuwa mwanataekwondo.

Mgeni rasmi katika mashindano hayo alikuwa ni Adan Mohammed, katibu mkuu kwenye idara ya elimu, masuala ya vijana na michezo katika serikali ya Kaunti ya Kilifi nchini Kenya.

Mashindano hayo ya siku moja ambayo yalishirikisha zaidi ya vilabu 10 vya wasichana na wavulana katika vitengo vya watu wakubwa, vijana na watoto yaliandaliwa kwenye ukumbi wa shule ya Pwani Secondary Vocational School for the deaf iliyoko katika Kaunti ya Kilifi nchini Kenya mwishoni mwa wiki iliyopita.

 

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin