Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

Handiboli: NCPD, Strathmore, Rising Starlets zaibuka kidedea ligi Handiboli Kenya

Na Anthony Aroshee

Jumatano, Septemba 25, 2019

Timu ya Bodi ya nafaka nchini NCPD, Strathmore na Rising Starlets zilifanikiwa kushinda mechi za ligi ya Taifa katika mchezo wa Mpira wa Mikono nchini Kenya upande wa Wanawake na Wanaume zilizochezwa Uwanjani Kaloleni eneo bunge la Makadara Kaunti ya Nairobi, mwishoni mwa juma lililopita.

Wikendi hiyo iliyopita, haikuwaendea vyema timu za National Youth Service na Mount Kenya University Thika kwani zilifanya vibaya kwa kupoteza mechi dhidi ya wapinzani wao katika kitengo cha ligi ya Wanawake.

Timu ya Bodi ya nafaka nchini yaani National Cereal Produce Board NCPB waliwalaza Mount Kenya University Thika MKU mabao 35-12 siku ya Jumamosi kabla ya kuwadunga Kenyatta University mabao 22-19 siku ya Jumapili iliyopita katika ligi ya Wanaume.

Kwa upande mwengine, timu ya Strathmore waliwatandika Warriors mabao 71-11 kabla ya kuwanyoosha National Youth Service NYS kwa kuwafumua mabao 41-18.

Kuhusu matokeo ya mechi nyingine zilizochezwa Jumamosi iliyopita, timu ya JKUAT pia walicheza mechi mbili. Kwanza waliwashinda Generation mabao 15-0 siku ya Jumamosi kabla ya kupoteza kwa Buccaneers walipokubali kufungwa mabao 22-20 katika mchezo uliofanyika Jumapili siku ambayo Inspired Boys waliwalemea NYS kwa kuwafunga mabao 25-23.

Black Mamba waliwafanya vibaya Warriors kwa kuwafunga mabao 64-11.

Na katika mechi za ligi ya kitengo cha Wanawake, Rising Starlets waling’ara kwa kushinda mechi mbili. Siku ya Jumamosi, walianza kuwafunga National Youth Service mabao 51-26 kisha wakamalizia kwa timu ya Mount Kenya University Thika MKU walipowachapa 37-27.

MKU Thika pia walipoteza mechi yao dhidi ya NCPB siku ya Jumamosi walipofungwa mabao 37-16 huku NYS pia vile vile wakipoteza mechi yao ya pili kwa kufungwa na mabingwa watetezi Nairobi water mabao 54-10.

 

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin