Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

Refa aliyempiga teke mchezaji asimamishwa kazi Ufaransa

Na Dawati La Michezo

Jumanne, Januari 16, 2018

Refa ambaye anadaiwa kumrushia teke mchezaji wa klabu ya Nantes nchini Ufaransa kabla ya kumfukuza uwanjani mechi yao dhidi ya Paris St-Germain amesimamishwa kazi.

Chama cha Soka cha Ufaransa kimetangaza kwamba amesimamishwa kazi kwa muda usiojulikana "hadi uamuzi mwingine utolewe."
Beki Diego Carlos alimgonga mwamuzi Tony Chapron kwenye kisigino katika kilichoonekana kama ajali tu dakika za mwisho za mechi.

Chapron alimrushia teke mchezaji huyo na kisha akampa kadi ya pili ya njano, kwa sababu ya kulalamika. PSG walishinda mechi hiyo 1-0.
Nantes wanataka kadi hiyo ibatilishwe kwani isipobatilishwa atakosa mechi moja.

FA ya Ufaransa imesema chama cha waamuzi kimeamua "kumuondoa Tony Chapron ambaye alikuwa ameteuliwa kusimamia mechi ya Ligue 1 Jumatano kati ya Angers na Troyes, hadi wakati mwingine".

Wameongeza: "Bw Tony Chapron karibuni ataitwa kukutana na kamati ya nidhamu ya LFP [Wasimamizi wa Ligi Ufaransa].
"Bw Tony Chapron, baada ya kutazama picha na video baadaye, alikiri kwamba aliangushwa kimakosa."

Mwenyekiti wa Nantes Waldemar Kita amesema Chapron anafaa kupigwa marufuku kwa miezi sita kwa sababu ya uamuzi huo wenye utata.
Ameongeza kuwa: "Sitaki kuamini kwamba alifanya hivyo makusudi."

"Ni mzaha," Kita aliambia runinga moja ya Ufaransa. "Nimepokea arafa 20 kutoka pande mbalimbali duniani kuniambia kwamba huyu mwamuzi ni mzaha tu.
"Nikizungumzia hili sana, nitaitwa kujibu maswali na kamati ya maadili. Hatuna haki ya kusema chochote."

Kwa Hisani Ya BBC

 

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin