Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

FKF Busia County League kuendelea tena Jumapili hii, kunapigwa mitanange miwili

Na Anthony Aroshee

Jumapili, Novemba 25, 2018

Klabu ya Airstrip Ajax FC wako nyumbani Jumapili hii ya Novemba 25 kumenyana na wageni wao timu ya Mabale FC katika mechi ya Ligi ya Kaunti ya Busia ya FKF tawi la Magharibi ya Shirikisho la Soka nchini Kenya.

Ngarambe hiyo itachezwa Busia County Stadium katika eneo bunge la Matayos.

Vijana wa Uwanja mdogo wa ndege wa Airstrip Ajax FC wa kutoka wadi ya Chakol Kusini, wanashuka dimbani kucheza mechi yao ya pili Jumapili hii baada ya kupata ushindi wa bwerere wa alama tatu na mabao 2-0 ugenini bila kugusa mpira dhidi ya wapinzani wao Budokomi FC ya kutoka wadi ya Bukhayo magharibi, waliokosa kufika Uwanjani.

Mchezo huo ulikuwa uchezwe Jumamosi iliyopita ya Novemba 24 kwenye Uwanja wa shule ya msingi ya Budokomi eneo bunge la Teso Kusini.

Matokeo hayo yaliifanya Airstrip Ajax FC kufikisha alama 46 wakiwa katika nafasi ya tano kutokana na mechi 25 huku wageni wao timu ya Mabale FC ya kutoka wadi ya Mayenje, wakiwa wa tisa kwa alama 27 baada ya kucheza mechi 24.

Mechi nyingine ya pili inayopepetwa Jumapili hii, ni ambao unawakutanisha wenyeji timu ya Mundulusia FC ya kutoka wadi ya Bukhayo, ambao wana alama 48 kwenye nafasi ya tatu, wanawakaribisha wageni timu ya Burumba Diamond FC katika Uwanja wa shule ya msingi ya Mundulusia huko Matayos.

Burumba Diamond waana alama 23 kwenye nafasi ya 11 katika jedwali ya ligi inayoongozwa na timu ya Busia Olympic FC kwa alama 54.

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin