Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

Yaounde yaanza vyema Ligi ya FKF Kwale County msimu 2019

Na Anthony Aroshee

Jumanne, Julai 2, 2019

Bao lililopachikwa wavuni na mshambuliaji hatari Antony Mwangeti liliiwezesha timu ya Yaounde FC kuinyuka Sorbibo FC bao 1-0 na kuanza vyema mkondo wa kwanza wa msimu mpya 2019 wa Ligi ya Kaunti ya Kwale Zone D ya Shirikisho la Soka nchini Kenya FKF tawi la Pwani Kusini.

Mwangeti alicheka na wavu kwa kuvurumisha mpira kimyani katika dakika ya 64 na kuhakikisha timu yake ya Yaounde FC, kutoka wadi Chengoni Samburu eneo bunge la Kinango, wanaondoka ugenini na alama tatu muhimu.

Mechi hiyo ya mkondo wa kwanza, ilipigwa Jumapili iliyopita ya Juni 30 kwenye Uwanja wa Mackinon.

Timu hizo zitarudiana katika mechi ya mkondo wa pili itakayofanyika Jumapili ya Julai 21, 2019 wakati Yaounde FC watakapowakaribisha wageni wao timu ya Sorbibo FC kwenye Uwanja wa Kasarani, ulioko Samburu huko Kinango.

Sorbibo FC watacheza mechi yao ya pili ugenini Jumamosi ijayo ya Julai 6 dhidi ya wenyeji wao Hot Desert FC kwenye Uwanja wa shule ya msingi ya Bahakwenu.

Nao vijana wa Yaounde FC, wanaonolewa na Kocha Mkuu Hamisi Mwagomba, watapumzika kwa muda wa majuma mawili kabla ya kucheza mechi yao ya pili dhidi ya wageni wao timu ya Hot DesertFC Jumapili ya Julai 14, 2019 katika Uwanja wa Kasarani ulioko Samburu.

Ligi hiyo ya Kaunti ya Kwale Zone D inashirikisha timu tatu.

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin