Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

Rais Uhuru Kenyatta azitaka Taifa Stars, Harambee Stars zitishe Afrika

Na Dawati La Michezo

Ijumaa, Julai 5, 2019

Rais wa Kenya Uhuru Muigai Kenyatta amezitaka timu za Soka za mataifa ya Kenya na Tanzania, zijipange upya ili zifanye vizuri zaidi katika Michuano mbali mbali ya Kimataifa barani Afrika.

Rais Kenyatta ametoa wito huo siku kadhaa baada ya Harambae Stars na Taifa Stars kubanduliwa nje kwenye hatua ya makundi ya Michuano ya makala ya 32 ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ya mwaka huu 2019 inayoendelea nchini Misri, na kushindwa kutinga hatua ya 16-Bora.

Rais Kenyatta aliyasema hayo Ijumaa hii ya Julai 5, 2019 akiwa kwenye ziara binafsi ya siku mbili katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo alipokewa na mwenyeji wake rais John Pombe Magufuli.

Akigusia vile Harambee Stars na Taifa Stars zilivyofanya katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON ya mwaka huu 2019 nchini Misri, rais huyo alisema sio jambo la kufurahisha kwa Harambee Stars na Taifa Stars kubanduliwa mapema na hivyo zinapaswa kujipanga ili ziwe zinafanya vizuri.

"Juzi tumechapana kule Cairo, kila mtu na timu yake. Harambee Stars na Taifa Stars ndio wao huko, nafikiri siku ile hakuna mtu aliyelala.
"Lakini hiyo ndiyo hali ya mchezo jamani.
Taifa Stars na Harambee Stars, ambazo zilikuwa pamoja katika Kundi C, zilishika nafasi mbili za mwisho kwenye kundi hilo. Harambee Stars waliwachapa Taifa Stars mabao 3-2 katika mchezo wa hatua ya makundi.

Katika ziara hiyo, rais Kenyatta akizungumza kwenye hadhara, hakusita kugusia matokeo ya mpambano huo.

"Tulishindana, safari hii Kenya ikagonga Taifa Stars. Lakini jamani hata nyie mlifaidika wakati tulipocheza na Senegal. Nyie mlichapwa mbili na sisi tulichapwa tatu.
"Kwa hiyo tujikakamue jamani. Turudi uwanjani sasa, mashindano hatutaki tuondolewe raundi ya kwanza. Fainali tukutane Kenya na Tanzania. Tanzania ikishinda na Kenya itashinda na Kenya ikishinda na Tanzania imeshinda si ndio jamani?' alisisitiza Rais Kenyatta.

Kwa upande wake rais Magufuli alisema, “Uhuru Kenyatta amekuja kuniomba msamaha kwa sababu ametufunga mabao 3-2, kwa sababu tulikubaliana tufungane magoli 2-2. Tulipofunga la pili sisi tukatulia yeye akaongeza la tatu, kwahiyo nikasema ngoja ni msubiri atakuja kuomba msamaha.” Alisema rais Magufuli

Ziara hiyo ya rais Kenyatta ni ya kuimarisha uhusiano wa kijirani baina ya Kenya na Tanzania huku marais hao wawili wa mataifa jirani wakikutana kwenye kijijini kwa rais Magufuli wilayani Chato katika mkoa wa Geita.

Rais Kenyatta anamaliza ziara hiyo Jumamosi hii ya Julai 6.

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin