Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

Marekani mabingwa tena Kombe la Dunia Wanawake

Na Dawati La Michezo

Jumatatu, Julai 8, 2019

Timu bora zaidi kwa kiwango duniani Marekani imefanikiwa kulihifadhi tena kwa mara ya pili mfululizo Kombe la Dunia la FIFA kwa Wanawake baada ya kuichapa Uholanzi mabao 2-0 katika mechi ya fainali iliyopigwa Jumapili iliyopita ya Julai 7, 2019 kwenye Uwanja wa Groupama, Decines-Charpieu ulioko Lyon, Ufaransa.

Bao la kwanza la Marekani lilipachikwa wavuni na nahodha Megan Rapinoe dakika ya 61 kwa njia ya mkwaju wa penalti kabla ya mchezaji Rose Lavelle kuhitimisha ushindi huo kwa kufunga bao la pili na la ushindi dakika ya 69 na kuliwezesha taifa lake la Marekani kutwaa taji hilo kwa mara yao ya Nne.

Sweden ilimaliza ya tatu baada ya kuishidna England mabao 2-1 katika mechi ya kumtafuta mshinde wa tatu na wa Nne.

Kufuatia ushindi huo wa timu ya Marekani, ambayo haijawai kumaliza chini ya nafasi ya tatu kwenye michuao ya Kombe la Dunia kwa Wanawake, imekuwa taifa la pili kufanikiwa kulihifadhi taji hilo la Dunia.

Wachezaji watatu Megan Rapinoe na Alex Morgan wote wa Marekani pamoja na Ellen White wa England, wamemaliza michuano hiyo wakiwa na mabao sita kila mmoja. Rapinoe ndiye aliyepata tuzo ya Mchezaji Bora wa michuano hiyo huku mlinda lango wa Uholanzi Sari Van Veenendaal alipata tuzo ya Mlinda Lango Bora.

Giulia Gwinn wa Ujerumani alikuwa mchezaji mwenye umri mdogo huku wenyeji Ufaransa wakipata tuzo ya timu iliyokuwa na nidhamu katika michuano hiyo.
Jumla ya mabao 124 yalifungwa katika mechi 52 zilizopigwa huku kadi 4 nyekundu zikionyeshwa wachezaji waliocheza vibaya Uwanjani.

Uholanzi mabingwa wa Ulaya, wameshiriki michuano ya Kombe la Dunia ya mwaka huu 2019 kwa mara ya pili baada ya kufanikiwa kufuzu kwenye michuano yao ya kwanza iliyoandaliwa mwaka 2015.

Michuano hiyo ya makala ya Nane ambayo ilianza rasmi Juni 7, 2019, ilifanyika kwenye miji tisa nchini Ufaransa ya Grenoble, Le Havre, Lyon, Montpellier, Nice, Paris, Reims, Rennes na Valenciennes.

Mataifa 24 yaliyogaanywa kwenye makundi sita ya timu Nne, yalichuana huku Afrika ikiwakilishwa na mataifa matatu Banyana Banyana ya Afrika Kusini waliokuwa wanashiriki kwa mara ya kwanza, The Indomitable Lionesses wa Cameroon na Super Falcons wa Nigeria walioshiriki kwa mara ya Nane.

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin