Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

Brazil yabeba Copa America yaiiadhibu Peru fainali

Na Dawati La Michezo

Jumanne, Julai 9, 2019

Brazil wamenyanyua Ubingwa wa Michuano ya Kombe la Copa America kwa kuichapa Peru mabao 3-1 katika mpambano wa fainali uliofanyika alfajiri ya kuamkia Jumapili iliyopita ya Julai 7, 2019 kwenye Uwanja wa Jornalista Mario Filho, au Maracana mjini Rio de Janeiro. ,

Brazil ilitangulia kufunga bao la kuongoza baada ya mchezaji Everton kuvuruisha mpira kimyani katika dakika ya 16 kabla ya Peru kusawazisha bao hilo lililofungwa na Paolo Guerrero kwa njia ya penalti dakika ya 44 baada ya beki wa kati wa Brazil Thiago Silva, kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.

Gabriel Jesus aliifungia Brazil bao la pili dakika ya 45 kabla ya kutolewa Uwanjani kwa kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 70 kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano. Bao la tatu la Brazil liliwekwa wavuni na Richarlison kwa mkwaju wa penalti kunako dakika ya 90.

Timu hizo zilikuwa katika Kundi moja la A pamoja na ambapo Brazil iliwapiga Peru ‘mukono’ mabao 5-0 mechi ya hatua ya makundi iliyochezwa majuma mawili yaliyopita, mjini Sao Paulo.

Brazil ilitinga fainali baada ya kuwatandika mahasimu wao wa jadi Argentina mabao 2-0 yaliyofungwa na Gabriel Jesus pamoja na Roberto Firmino katika mechi ya Nusu fainali iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uwanja wa Governador Magalhaes Pinto, Belo Horizonte, Minas Gerais.

Nayo Peru iliicharaza Chile mabao 3-0 katika mechi nyingine ya Nusu fainali.

Nayo Argentina ilichukua nafasi ya tatu baada ya kuifunga Chile mabao 2-1 kwenye mchezo wa kumtafuta mshinde wa tatu wa michuano hiyo ya Copa America huku mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi akionyeshwa kadi nyekundu ya pili katika maisha yake ya soka.

Mara ya mwisho Brazil kushinda Kombe la Copa America ilikuwa mwaka 2007 ilipokuwa mwenyeji wa michuano hiyo inayoshirikisha mataifa ya Bara la Marekani ya Kusini.
Taji hilo ni la tisa kwa Brazil kunyanyua katika historia yake ya Kombe la Copa America.

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin