Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

Lionel Messi adinda kuchukua medali ya nafasi ya tatu Copa America

Na Dawati La Michezo

Jumanne, Julai 9, 2019

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina, ambaye pia ndiye nahodha wa kikosi hicho Lionel Messi, hakuonekana jukwaani wakati wa kuchukua medali za mshindi wa tatu katika Michuano ya Copa America inayoshiriki mataifa ya Bara la Marekani ya Kusini.

Argentina ilimaliza ya tatu baada ya kuishinda Chile mabao 2-1 katika mechi ya kumtafuta mshinde wa tatu kwenye mchezo ambao nyota huyo wa Barcelona, alionyeshwa kadi nyekundu na kutoka nje ya Uwanjani na hakurudi tena.

Katika mchezo huo, Messi na mwenzie Gary Medel wa Chile, waliotolewa nje ya Uwanja baada ya mwamuzi wa mechi hiyo Mario Diaz de Vivar kuwaonyesha kadi nyekundu baada ya wanandinga hao kutunishiana misuli Uwanjani.

Messi hakufurahia na kitendo hicho akisisitiza kuwa ulikuwa ni muendelezo wa upendeleo unaofanywa na Shirikisho la Soka la Amerika Kusini CONMEBOL ambao pia ndio waandaaji wa michuano hiyo ya Copa America.

Hiyo ilikuwa ni kadi nyekundu ya pili Messi kupata katika maisha yake ya soka tangu mwaka 2005 alipopata kadi nyekundu ya kwanza.

Akielezea sababu za kutochukua medali hiyo, Lionel Messi amesema kuwa ni masuala ya rushwa yaliyogubika michuano hiyo, Huku akieleza kuwa kuna baadhi ya timu tayari zimeshatangazwa ubingwa hata kabla ya kucheza.

“Sijaenda kuchukua medali kwa sababu sitaki kuwa mmoja ya wala rushwa, Brazil watashinda mchezo wao wa fainali. Kwani fainali hiyo tayari imeshapangwa na ni muda tu ndio unaosubiriwa na mimi daima nitaendelea kuongea ukweli,’’ ameeleza Messi kwenye mahojiano yake na waandishi wa habari baada ya mpambano huo kumalizika.

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin