Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

Allan Wanga astaafu Soka ya Kimataifa

Na Dawati La Michezo

Jumanne, Julai 9, 2019

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Soka ya Kenya Harambee Stars Allan Wetende Wanga ametangaza kuustafu kucheza soka ya Kimataifa akiwa na umri wa miaka 33.

Wanga aliitumikia Harambee Stars kwa kipindi cha miaka 12 na kuifungia jumla ya mabao 22.

Mwanandinga huyo ambaye ni Mkurugeniz wa Michezo katika Kaunti ya Kakamega nchini Kenya, ameamua kuchukua hatua hiyo lakini ataendelea kuichezea klabu ya Kakamega Homeboyz FC inayoshiriki kwenye Ligi Kuu ya Kenya ya SportPesa.

Wanga anastaafu mwezi mmoja baada ya Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Harambee Stars Sébastien Migné kumtema kutoka katika kikosi kamili kilichoshiriki kwenye Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON mwaka huu 2019 nchini Misri.

Wanga ambaye pia alizichezea Tusker FC na AFC Leopards FC kwenye Ligi Kuu nchini Kenya, alimaliza wa pili katika ufungaji wa mabao mengi baada ya msimu uliopita wa Ligi Kuu nchini Kenya kukamilika, akiwa na mabao 18.

Alianza kuichezea Harambee Stars Mei 27, 2007 katika mechi ya kirafiki dhidi ya Super Eagles ya Nigeria huku akifunga bao lake la kwanza Kenya ikipoteza mabao 2-1 dhidi ya Taifa Stars Desemba 8, 2007 kwenye michuano ya Senior Challenge Cup.

Mshambuliaji huyo pia aliwai kucheza soka ya kulipwa nchini Angola katika klabu ya Petro Atlético ya Luanda, FC Baku nchini Azerbaijan, Hoàng Anh Gia Lai ya Vietnam, Al-Merrikh nchini Sudan kabla ya kumalizia nchini Tanzania Bara katika klabu ya Azam FC.

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin