Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

Antoine Griezmann atua Nou Camp akitokea Atletico Madrid

Na Dawati La Michezo

Ijumaa, Julai 12, 2019

Barcelona imemsajili mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa na klabu ya Atletico Madrid Antoine Griezmann, mwenye umri wa miaka 28, kwa mkataba wa miaka mitano baada ya kumwinda mchezaji huyo kwa muda wa miaka miwili iliyopita.

Griezmann, ambaye yuko likizo kwenye kisiwa cha Ibiza nchini Uhispania, amemwaya wino akiwa ndani ya mashua.

Uhamisho huo umewagharimu mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Uhispania ya La Liga Barecelona, kitita cha Pauni milioni 108 na kuweka sharti la pauni milioni 717 kwa klabu yeyote itakayotaka kumsajili Griezmann kutoka Nou Camp.

Mfaransa huyo alimwaya wino wa mkataba mpya wa miaka mitano mwezi Juni 2018 wa kuendelea kuitumikia Atletico Madrid, hata hivyo ilipofika mwezi Mei 2019, akatangaza kuwa ataondoka klabuni humo katika dirisha la usajili la majira haya ya joto.

Mshambuliaji huyo ni mshindi wa Kombe la Dunia la FIFA akiwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa kilichonyanyua taji hilo katika michuano iliyoandaliwa Urusi mwaka jana 2018.

Griezmann alijiunga na Atletico Madrid akitokea Real Sociedad mwaka 2014 na ameipachikia Atletico Madrid jumla ya mabao 133 katika mechi 257 alizocheza katika muda wa miaka mitano na sasa anakuwa mchezaji wa sita ghali zaidi duniani kusajiliwa nyuma ya Neymar, Kylian Mbappe, Philippe Coutinho, Joao Felix na Ousmane Dembele.

 

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin