Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

Al Ahly, Bafana Bafana, Royal Club kushuka dimbani Ligi ya FKF Div Two Northern Zone Pool B wikendi hii

Na Anthony Aroshee

Ijumaa, Julai 12, 2019

Jumla ya mechi 14 za Ligi ya Taifa Daraja la Pili Kanda ya Kaskazini ya Kundi B ya Shirikisho la Kabumbu nchini Kenya FKF, zimeratibiwa kupigwa mwishoni mwa juma hili kwenye viwanja mbali mbali kuanzia alasiri saa 15:00hrs(EAT).

Mechi sita zinachezwa Jumamosi hii ya Julai 13 kabla ya kusakatwa mechi nyingine saba siku ya Jumapili ya Julai 14, 2019 huku Muli Children's Family(MCF FC), ambao wako katika nafasi ya pili kwa alama 54, wanacheza mechi mbili za nyumbani kwenye Uwanja wao wa Matuu.

Kwanza wanawaalika Bafana Bafana FC Jumamosi hii kabla ya kumaliza udhia na timu inayoshikilia nafasi ya sita kwa alama 41 Isiolo Youth FC, siku ya Jumapili. Bafana Bafana FC, wenye alama 30 katika nafasi ya 12, watashuka tena dimbani siku ya Jumapili kuwakabili vinara wa ligi hiyo Machakos United FC katika Uwanja wa Machakos.

Machakos United wako kileleni mwa jedwali wakiwa na alama 55.

Na kwenye Uwanja wa Kitengela Road Block, wenyeji wa uga huo timu ya Kitengela Allstars FC, wenye alama 49 katika nafasi ya tatu, Jumamosi wanawakaribisha wageni Mwingi Junior Stars(MJS FC) kisha wapambane na timu ya wanafunzi wa Daystar University FC siku ya Jumapili.

Timu hiyo ya Daystar University FC, ambao wana alama 31 wakiwa katika nafasi ya 11, Jumamosi hii wako ugenini dhidi ya wenyeji Flora FC katika Uwanja wa Isinya. Flora FC wenye alama 32 kwenye nafasi ya 10, watacheza ugenini Jumapili kuvaana na Kitengela Sportiff FC kuanzia mchana saa 13:00hrs(EAT) katika Uwanja wa Kitengela Road Block.

Nayo Royal Club FC inayoshikilia nafasi ya Nne kwa alama pia 49 Jumamosi wako ugenini kuchuana dhidi ya wenyeji Kitengela Sportiff FC kwenye Uwanja wa Kitengela Road Block, mechi ambayo itaanza mchana saa 13:00hrs(EAT).

Kitengela Sportiff FC wako katika nafasi ya 13 wakiwa na alama 27.

Na kwenye Uwanja wa Mwingi, wenyeji Super Solico FC wenye alama 33 katika nafasi ya tisa, wataanza kupepetana na Meru Mutindwa Bombers FC kabla ya kufunga kazi siku ya Jumapili dhidi ya wageni wao Dummen Orange FC, ambao Jumamosi wanacheza ugenini na timu Al Ahly FC Uwanjani Kajiado.

Dummen Orange FC wako kwenye nafasi ya saba wakiwa na alama 39 huku Meru Mutindwa Bombers FC, ambao wametulia kwenye nafasi ya nane kwa alama 34, wakishuka tena dimbani ugenini Jumapili kupambana na wenyeji wao Mwingi Junior Stars(MJS FC) Uwanjani Mwingi.

Al Ahly FC, ambayo inakamata nafasi ya tano baada ya kujikusanyia jumla ya alama 47, Jumapili pia watakuwa nyumbani kumaliza wikendi kwa kukwatuana na Tonny Coren Gategi FC katika Uwanja wa Kajiado.

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin