Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

AFCON 2019: Nigeria na Tunisia kuwania nafasi ya tatu Jumatano hii

Na Dawati La Michezo

Jumatano, Julai 17, 2019

Super Eagles ya Nigeria na The Carthage Eagles ya Tunisia wanapambana Jumatano hii ya Julai 17, 2019 katika mechi ya kumtafuta mshinde wa tatu kwenye Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2019.

Patashika hiyo, ambayo itaanza usiku saa 10:00hrs(EAT), itachezwa kwenye Uwanja wa Al Salam jijini Cairo, Misri huku timu hizo zikikutana baada ya kushindwa katika mechi za hatua ya Nusu fainali zilizopigwa Jumapili ya Julai 14, jijini Cairo.

Safari ya Tunisia, mabingwa wa AFCON mwaka 2004 kutaka kulishinda taji la AFCON kwa mara ya pili, ilitamatika baada ya kupoteza kwa Simba wa Teranga wa Senegal bao 1-0 katika mechi ya kwanza ya nusu fainali huku Nigeria, mabingwa mara tatu wa taji la AFCON, wakifungwa na Algeria mabao 2-1 katika mechi ya pili ya nusu fainali.

Tunisia imecheza mechi ya saba ya hatua ya Nusu fainali katika historia ya michuano ya AFCON.

Nigeria, inayofunzwa na Kocha Gernot Rohr, wanashiriki michuano ya AFCON ya mwaka huu 2019 kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2013 wakati waliposhinda taji hilo kwa mara ya tatu.

Nigeria na Tunisia wameshakutana mara 18 katika mechi za awali. Tunisia imeshinda mechi sita ilhali Nigeria imeibuka mshindi mara tano huku timu hizo zikitoka sare mara saba.

Lakini katika michuano ya AFCON, mara ya mwisho mataifa hayo kukutana, ilikuwa mwaka 2006 nchini Misri kwenye mchezo wa Robo fainali ambao Nigeria walishinda kwa njia ya mikwaju ya penalti na kutinga Nusu fainali baada ya timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 katika muda wa kawaida.

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin