Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

Kagame Cup: Azam yatangulia nusu fainali

Na Dawati La Michezo

Jumatano, Julai 17, 2019

Mabingwa watetezi wa Michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame Azam FC kutoka Tanzania Bara, wamefuzu kwenye hatua ya Nusu fainali baada ya kuifunga TP Mazembe mabao 2-1 katika mechi ya Robo fainali iliyopigwa Jumanne iliyopita nchini Rwanda

TP Mazembe ndio walianza kupata bao la kuongoza kupitia kwa Ipyamy Giovani dakika 21 kabla ya Azam FC kurudisha bao hilo dakika saba baadae lililofungwa na Idd Seleman ‘Nado’. Bao la pili na la ushindi la Azam FC lilipachikwa kimyani na mshambuliaji Obrey Chirwa

Azam FC, yenye makao yake jijini Dar es Salaam, walipangwa katika Kundi B pamoja na wenyeji Mukura Victory, KCCA ya Uganda na Bandari kutoka Mombasa nchini Kenya huku TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wakijumuishwa kwenye Kundi A na wenyeji Rayon Sports, Atlabara ya Sudan Kusini na KMC ya jijini Dar es Salaam Tanzania.

Azam FC wanawania kutwaa taji la tatu mfululizo la Kombe la Kagame katika michuano ya mwaka huu, baada ya awali kulichukua mara mbili mfululizo wakati michuano hiyo ilipoandaliwa nyumbani, Tanzania.

Azam FC walibeba taji hilo kwa mara ya kwanza mwaka 2015 baada ya kuwafunga mabingwa wa Ligi Kuu ya Kenya K’Ogalo Gor Mahia ya Kenya 2-0 yaliyofungwa na John Bocco dakika ya 17 na Kipre Herman Tchetche dakika ya 64 katika mchezo wa fainali uliochezwa Agosti 2 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Wakatetea taji hilo Julai 13 mwaka jana 2018 jijini Dar es Salaam kwa kuwashinda wekundu wa msimbazi mnyama Simba SC mabao 2-1 huku Azam FC wakipata mabao yao kupitia mshambuliaji Shaaban Iddi Chilunda dakika ya 33 na beki Aggrey Moris dakika ya 69. Bao la Simba SC lilivurumishwa wavuni na mshambuliaji Kagere Meddie dakika ya 63.

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin