Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

FKF Kwale County League: Lunga Lunga Cranes na Perani FC watoka sare

Na Anthony Aroshee

Jumatano, Julai 17, 2019

Timu ya Lunga Lunga Cranes FC walilazimishwa kutoa sare ya 2-2 mbele ya mashabiki wao katika mechi ya nyumbani dhidi ya wageni Perani FC kwenye mpambano wa mwisho wa kumaliza mkondo wa kwanza wa Ligi ya Kwale County Kundi A msimu huu 2019 ya Shirikisho la Kabumbu nchini Kenya FKF tawi la Pwani Kusini.

Patashika hiyo ya kihistoria, ilipigwa Jumapili iliyopita ya Julai 14, 2019 kwenye Uwanja wa shule ya Sekondari ya Lunga Lunga ulioko kwenye eneo bunge la Lunga Lunga ikiwa ni mechi ya kwanza ya FKF kuchezwa katika eneo hilo kwa muda wa miaka 20 iliyopita.

Mchezaji Mohammed Mzungu wa Lunga Lunga Cranes FC ndiye aliyetangulia kuwanyanyua mashabiki wa nyumbani kwa kufunga bao la kuongoza dakika ya 65. Bao hilo lilidumu kwa muda wa dakika Nne tu kabla ya mchezaji Hakim Kimbonja wa Perani FC kurudisha bao hilo kunalo dakika ya 69.

Perani FC walichukua uongozi wa mpambano huo baada ya mchezaji Bakari Mbovu kuuweka mpira nyuma ya nyavu katika dakika ya 75. Lakini vijana wa Lunga Lunga Cranes FC walifanikiwa kusawazisha bao hili dakiak dakika tano baadae kupitia mchezaji Salim Mwadadu.

Kutokana na matokeo hayo, Perani FC wamemaliza mkondo wa kwanza wa ligi hiyo ya FKF Kwale County Kindi A wakiwa katika nafasi ya pili kwa alama Nne baada ya kushuka dimbani mara tatu.

Nayo Lunga Lunga Cranes FC wamemaliza wakivuta mkia baada ya kuambulia alama moja tu katika msimamo wa kundi hilo linaloshirikisha timu Nne.

Mkondo wa pili wa ligi hiyo, unaanza mwishoni mwa wikendi hii huku Lunga Lunga Cranes FC wakisafiri ugenini huko Mwabungo kuwakabili wenyeji wao Real Junior FC ilhali Eleven Stars FC watawaalika wageni wao Perani FC kwenye Uwanja wa Mwabungo Dico Star.

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin