Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

AFCON 2019: Simba wa Teranga wanakutana na Mbweha wa Jangwani

Na Dawati La Michezo

Ijumaa, Julai 19, 2019

Afrika Magharibi inakutana na Afrika Kaskazini katika mpambano wa kufunga rasmi pazia la Michuano ya Makala ya 32 ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON ya mwaka huu 2019 usiku huu wa Ijumaa ya Julai 19, jijini Cairo nchini Misri kwa kuandaliwa fainali ya kukata na shoka.

Kipute hicho kinawakutanisha Simba wa Teranga wa Senegal na Mbweha wa Jangwani wa Algeria kitakachoanza usiku saa 10:00hrs(EAT) kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Cairo, unaoweza kuwaingiza mashabiki wapatao 75,000.

Senegal, wanaonolewa na Kocha mzalendo Aliou Cisse, walifuzu fainali kwa kuwanyuka The Carthage Eagles wa Tunisia bao 1-0 katika muda wa ziada kwenye mchezo wa kwanza wa Nusu fainali uliotamatika bila kufungana katika muda wa ziada nao Algeria walitinga fainali baada ya kuwafunga Super Eagles ya Nigeria mabao 2-1 katika mechi nyingine ya Nusu fainali.

Riyad Mahrez aliifungia Algeria bao la ushindi kupitia mpira wa freekick dakika tano ya muda wa majeruhi.

Algeria na Senegal walimaliza wa kwanza na wapili mtawalia baada ya mechi za hatua ya makundi na kutinga katika raundi ya mtoano. Timu hizo, zote zilikuwa kwenye Kundi C pamoja na Harambee Stars ya Kenya na Taifa Stars ya Tanzania huku Algeria wakishinda mechi zao zote za hatua ya makundi.

Kwanza waliwatandika Kenya mabao 2-0 kisha wakawanyuka Senegal bao 1-0 kabla ya kuwacharaza Tanzania mabao 3-0 na kuongoza kundi hilo kwa alama tisa huku Senegal, ambao waliwafunga Tanzania mabao 2-0 na Kenya mabao 3-0, wakimaliza wa pili wakiwa na alama sita.

Kwenye hatua ya mtoano, Senegal waliwafunga Uganda Cranes bao 1-0 wakati Algeria wakiichapa Guinea mabao 3-0 na kutinga hatua ya Robo fainali ambapo Senegal waliwafunga Benin bao 1-0 nao Algeria wakawashinda Ivory Coast mabao 4-3 kupitia mikwaju ya penalti baada ya sare ya bao 1-1 katika muda wa kawaida.

Mbweha wa Jangwani wa Algeria wanawinda Kombe la AFCON kwa mara ya pili baada ya kushinda taji hilo miaka 29 iliyopita wakiwa wenyeji kwa kuwafunga Nigeria bao 1-0 katika mechi ya fainali ya michuano ya makala ya 17 mwaka 1990, ikiwa ni fainali ya pili kucheza kwenye michuano hiyo.

Fainali ya kwanza Algeria kucheza, walizabwa na Nigeria mabao 3-0 kwenye michuano ya makala ya 12 iliyoandaliwa nchini Nigeria mwaka 1980.

Simba wa Teranga wa Senegal, ambao hawajawai kushinda taji la AFCON baada ya miaka 54 kujaribu, wametinga fainali kwa mara ya pili baada ya miaka 17 walipopoteza kwa Cameroon mabao 3-2 kwa njia ya mikwaju ya penalti baada ya timu hizo kutoka sare ya bila kwa bila katika fainali ya michuano ya makala ya 23, iliyofanyika nchini Mali mwaka 2002. Kikosi cha Senegal wakati huo kiliongowa na nahodha, Aliou Cisse.

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin