Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

AFCON 2019: Bingwa kuzawadiwa kitita cha USD 4.5 Million

Na Dawati La Michezo

Ijumaa, Julai 19, 2019

Mabingwa wa mwaka huu 2019 wa Michuano ya Makala ya 32 ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON, licha na kushinda taji hilo, pia atajishindia kima cha fedha kutoka kwa wadhamini wakubwa wa michuano hiyo, Kampuni ya Total.

Timu itakayoibuka bingwa, itapata kitita cha Dola za Marekani 4.5 million (KSh456 million) huku mshinde wa pili, akiondoka na Dola 2.5 million (KSh253 million).

Fainai ya mwaka huu 2019 ni kati ya Simba wa Teranga wa Senegal na Mbweha wa Jangwani wa Algeria inayopigwa usiku huu wa Ijumaa Julai 19, 2019 kuanzia saa 10:00hrs(EAT) kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Cairo, wenye uwezo wa kubeba mashabiki zaidi ya 75,000 uliofunguliwa mwaka 1960.

Nazo timu zilizoshindwa katika hatua ya Nusu fainali, Nigeria na Tunisia, kila mmoja itakabidhiwa Dola 2 million (KSh202 million) huku timu zilizopoteza kwenye mechi za robo fainali, zitapata Dola 800,000 (KSh81 million) ambazo ni Afrika Kusini, Ivory Coast, Madagascar na Benin.

Senegal, chini ya Kocha Aliou Cisse itakuwa inasaka taji lake la kwanza, kwani haijawahi kutwaa ubingwa wa michuano hiyo licha ya mwaka 2002, kutinga fainali ambayo walifungwa na Cameroon mabao 3-2 kwa mikwaju ya penalti.

Fainali ya mwaka 2002 ina kumbukumbu mbaya kwa Kocha Cisse kwani alikuwa miongoni mwa wachezaji waliokosa penalti huku akiwa nahodha. Ikumbukwe Cisse kwa kuingia tu hatua ya fainali ameweka rekodi ya kushiriki michuano miwili mikubwa akiwa kama kocha na mchezaji kwa nyakati tofauti.

Ameshiriki michuano ya Kombe la Dunia la FIFA mwaka 2002 nchini Korea Kusini na Japan akiwa mchezaji na mwaka 2018 nchini Urusi akiwa Kocha Mkuu, pia ameshiriki AFCON mwaka 2002 na 2004 akiwa mchezaji na mwaka huu akiwa kama kocha.

Naye Kocha Mkuu Djamel Belmadi wa Algeria, anakibarua cha kushinda taji la AFCON akiwa kama kocha baada ya kushindwa kutwaa pindi alipokuwa mchezaji wakiishia hatua ya robo fainali mwaka 2004 nchini Tunisia akiwa nahodha.

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin