Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

Omax FC yatoa ‘kipigo kizito’ yaichinja Kishada Ligi ya FKF Pwani Kusini

Na Anthony Aroshee

Jumapili, Julai 21, 2019

Timu ya Omax FC wamepata ushindi mnono wa mabao 3-1 ugenini baada ya kuwachabanga wenyeji wao timu ya Kishada FC katika mechi ya mwisho ya Kundi C ya msimu huu 2019 wa Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Kenya FKF Tawi la Pwani Kusini.

Patashika hiyo ya mkondo wa pili, imechezwa Jumapili hii ya Julai 21, 2019 kwenye Uwanja wa Freretown eneo bunge la Nyali katika Kaunti ya Mombasa huku vijana wa Omax FC, wanaopewa hamasa na Kocha Mkuu Ismail ‘Bokasa’ Abdalla, wakitangulia kufunga bao la kuongoza kwa kucheka na wavu kupitia mchezaji Ali Mzee kwa kuvurumisha mpira kimyani dakika ya 24.

Muda mfupi kabla ya timu hizo kwenda mapumzikoni, mchezaji Ibrahim Mdogo wa Omax FC aliwashangaza mashabiki wa Kishada FC kwa kupachika wavuni bao la pili kunako dakika ya 40 kabla ya Fadhil Ali kufunga bao la tatu dakika Nne baadae na kuifanya Omax FC kuongoza kwa mabao 3-0 katika kipindi cha kwanza.

Katika kipindi cha pili timu ya Kishada FC, inayofunzwa na Kocha Mkuu Athuman 'Israel' Mwishee, ilijipatia bao la kujifariji lililofungwa na Baya Juma kwenye dakika ya 54.

Omax FC imefanikiwa kulipiza kisasi cha kufungwa na Kishada FC bao 1-0 lililofungwa na Ali Ibrahim dakika ya 80 katika mechi ya mkondo wa kwanza iliyopigwa miezi mitatu iliyopita(Aprili 21, 2019) kwenye Uwanja wa shule ya msingi ya Ronald Ngala(RG Ngal).

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin