Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

Green Forest yapata ‘Walk-over’ Dragon ‘yaingia mitini’ Ligi ya FKF Pwani Kusini

Na Anthony Aroshee

Jumapili, Julai 21, 2019

Timu ya Green Forest FC kutoka Kinango Kaunti ya Kwale, imerudi nyumbani kutoka mjini Mombasa ikiwa na alama tatu na mabao mawili kibindoni baada ya kupata ushindi wa bwerere wa 2-0 dhidi ya wenyeji timu ya Dragon FC.

Mechi hiyo ya mwisho ya Kundi C ya msimu huu 2019 wa Ligi ya Shirikisho la Soka nchini Kenya FKF Tawi la Pwani Kusini, ilikuwa imepangwa kupepetwa Jumapili hii ya Julai 21, 2019 kwenye Uwanja wa Ziwani Lasco.

Lakini kipute hicho hakikuchezwa baada ya kikosi cha Dragon FC kutofika Uwanjani na kusababisha wageni Green Forest kupata ushindi wa chee wa mabao 2-0 bila kugusa mpira.

Hii ni mara ya pili kwa Green Forest FC kupata ‘Walk-over’ ya pili yaani ushindi wa bwerere dhidi ya timu ya Dragon FC ambayo haikusafiri kuwafuata wenyeji wao Green Forest FC katika mechi ya mkondo wa kwanza, iliyokuwa ichezwe Aprili 21, 2019 kwenye Uwanja wa shule ya msingi ya Mnyenzeni.

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin