Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

TUM Dynamos yaigeuza Sargoi Youth ‘mboga mchicha’ Ligi ya FKF Pwani Kusini

Na Anthony Aroshee

Jumapili, Julai 21, 2019

TUM Dynamos FC imeisambaratisha timu ya vijana ya Sargoi Youth FC kwa kuichapa mabao 2-0 katika mechi ya mwisho ya Kundi C msimu huu 2019 wa Ligi ya Shirikisho la Kabumbu nchini Kenya FKF Tawi la Pwani Kusini.

Mabao hayo ya washindi, yamefungwa na Brian Murage na Abdulmalik Black kwenye mchezo huo wa mkondo wa pili, uliosakatwa Jumapili hii ya Julai 21, 2019 kwenye Uwanja wa shule ya msingi ya Ronald Ngala(RG Ngala).

Murage ndiye aliyekuwa wa kwanza kufunga mapema kabisa bao la kuongoza dakika ya Nne tangu mpambano uanze huku Black akihitimisha ushindi huo kwa kufunga bao la pili na la ushindi dakika mbili baada ya kipindi cha pili kuanza.

Sargoi Youth FC, inayofunzwa na Kocha Omar Mafudh, ilipata alama moja ugenini dhidi ya wenyeji TUM Dynamos FC katika mechi ya mkondo wa kwanza iliyochezwa Aprili 22, 2019 kwenye Uwanja wa TUM.

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin