Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

Omax FC yatamba ni vinara wa Kundi C Ligi ya FKF Pwani Kusini

Na Anthony Aroshee

Jumapili, Julai 21, 2019

Klabu ya Omax FC wamemaliza Ligi baada ya kujikusanyia jumla ya alama 25 sawa na Kishada FC, wanaofuata katika nafasi ya pili, na kuongoza Kundi C msimu huu wa 2019 katika Ligi ya Shirikisho la Kandanda nchini Kenya FKF Tawi la Pwani Kusini.

Omax FC imefikisha alama hizo baada ya kushuka dimbani mara 10 ikishinda mechi Nane ikipoteza mchezo mmoja na kutoa sare mechi moja sawa na Kishada FC, ambayo inafuata katika nafasi ya pili ikiwa pia na alama 25 lakini imezidiwa kete na Omax FC kwa ubora wa mabao.

Katika tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa, Omax FC ina mabao 20 ilhali Kishada FC ina mabao 19. Hatahivyo, timu hizo zote mbili zimefuzu kucheza katika ‘Mini-Ligi’ ya FKF kutokana na kumaliza katika nafasi ya kwanz ana pili mtawalia.

TUM Dynamos FC imemaliza katika nafasi ya tatu kwa alama 15 alama mbili zaidi ya Green Forest iliyoridhika kwenye nafasi ya Nne huku Sargoi Youth FC ikitulia katika nafasi ya tano baada ya kuambulia alama tano.

Black Dragon FC ndio inayofuta mkia katika nafasi ya mwisho ya sita ikiwa na alama zao tatu baada ya kushinda mechi moja na kupoteza mechi tisa, kati ya mechi hizo ilizopoteza, haikuenda Uwanjani kucheza mechi tatu ilipeana ushindi wa bwerere(walk-over) kwa timu pinzani.

Green Forest FC ilipata ushindi wa mechi mbili za bwerere, nyumbani na ugenini dhidi ya Black Dragon FC huku Kishada pia ilipata ‘walk-over’ moja kutoka kwa Black Dragon.

Katika mechi za mwisho za mkondo wa pili kumaliza Kundi C, zilizogaragazwa Jumapili ya Julai 21, 2019, Omax FC ilimalizia ugenini kwa kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Kishada FC Uwanjani Freretown, eneo bunge la Nyali Kaunti ya Mombasa.

Nayo TUM Dynamos FC pia ilimalizia ugenini kwa kuichapa Sargoi Youth FC mabao 2-0 kwenye Uwanja wa shule ya msingi ya Ronald Ngala(RG Ngala) huku Green Forest FC ikipata ushindi wa bwerere ugenini wa alama tatu na mabao mawili baada ya wenyeji wao Black Dragon FC kutofika Uwanjani Ziwani Lasco mjini Mombasa.

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin