Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

Man City washinda taji la kwanza msimu mpya mabingwa wa Ngao ya Jamii

Na Dawati La Michezo

Jumatatu, Agosti 5, 2019

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Uingereza EPL, Manchester City ndio mabingwa wa Ngao ya Jamii msimu 2019/2020 baada ya kuwalaza mabingwa wa Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya Liverpool mabao 5-4 kupitia mikwaju ya penalti.

Man City wamehifadhi tena Ngao hiyo ya Jamii kwa mara ya pili mfululizo baada ya kulitwaa msimu 2017/2018.

Mikwaju ya matuta ilibidi kutumika kumpata bingwa baada ya klabu hizo kutoka sare ya bao 1-1 katika muda wa kawaida kwenye mpambano huo wa kufungua pazia la ligi kuu ya EPL, uliochezwa Jumapili iliyopita mbele ya umati mkubwa wa mashabiki Uwanjani Wembley, jijini London.

Kiungo mshambuliaji Raheem Sterling alianza kuifungia Manchester City bao dakika ya 23 akimalizia pasi kutoka kwa David Silva huku vijana wa Kocha Mjerumani Jurgen Klopp wakisawazisha kupitia Joel Matip dakika ya 77 akimalizia pasi ya beki Virgil van Dijk.

Katika upigaji wa mikwaju ya matuta, Man City walifunga penalti zao zote kupitia Ilkay Gundogan, Bernardo Silva, Phil Foden, Oleksandr Zinchenko na Gabriel Jesus huku Liverpool wakifunga matuta yao kupitia Xherdan Shaqiri, Adam Lallana, Alex Oxlade-Chamberlain na Mohamed Salah, wakati Georginio Wijnaldum alikosa kufunga tuta lake lililookolewa na kipa wa Man City, Claudio Bravo.

Manchester City walifanikiwa kushinda Ubingwa wa EPL msimu uliopita 2018/2019 kwa alama 98 alama moja zaidi ya wapinzani wao Liverpool huku wakimaliza msimu kwa kushinda mataji matatu katika msimu mmoja. Vijana hao wa Kocha Pep Guardiola, walishinda mataji mengine mawili, Kombe la FA na lile Kombe la Ligi.

Liverpool walimaliza msimu kwa kushinda taji la Michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuwashinda Tottenham Hotspurs.

 

 

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin