Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

CHAN 2020: Taifa Stars sasa kupambana na Sudan

Na Dawati La Michezo

Jumatatu, Agosti 5, 2019

Baada ya kuibandua nje Harambee Stars ya Kenya, timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' sasa watamenyana na Sudan katika mechi ya hatua ya mwisho ya mchujo kuwania tiketi ya kushiriki kwenye Michuano ijayo ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wanaocheza ligi ya Ndani(CHAN).

Taifa Stars wataanzia nyumbani Septemba 20, 2019 dhidi ya wageni wao Sudan kabla ya kumalizia ugenini Oktoba 18, jijini Khartoum katika raundi hiyo ya pili na ya mwisho ya kufuzu.

Tanzania ilitinga hatua ya pili baada ya kuwalaza Kenya mabao 4-1 kwa njia ya mikwaju ya penalti katika mechi ya marudiano iliyopiga Jumapili iliyopita kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Michezo wa Moi Kasarani, jijini Nairobi.

Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya 0-0 katika dakika 90 ambapo katika mechi ya mkondo wa kwanza uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, timu hizo pia zilitoka sare ya bila kufungana.

Penalti za Taifa Stars zilifungwa na Paul Godfrey 'Boxer', Erasto Nyoni, Gadiel Michael na Salum Aiyee huku Harambee Stars wakifunga penalti yao moja ambayo ilipigwa na Cliffton Miheso.

Kipa mkongwe wa Taifa Stars Juma Kaseja, aliyerejeshwa kikosini baada ya miaka sita, aliokoa tuta la Michael Kibwage huku penalti nyingine ya Kenya, ikipotezwa na Joash Achieng Onyango.

Michuano ya kuwania taji la CHAN kwa wachezaji wanaocheza soka katika ligi za nyumbani Afrika, itaandaliwa mwaka ujao 2020 nchini Cameroon ikishirikisha mataifa 16.

Mataifa hayo yatafuzu kutoka kanda zote za mchezo wa soka barani Afrika. Eneo la Afrika Mashariki na Kati, litatoa mataifa mawili yatakayofuzu.

Michuano ya kwanza ya CHAN iliandaliwa mwaka 2009 nchini Ivory Coast na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo(DRC) walishinda Ubingwa wa kwanza.
Morocco ndio iliyokuwa mwenyeji wa michuano ya mwisho mwaka 2018.

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin