Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

CECAFA Challenge U20 inaanza Jumamosi hii Uganda

Na Dawati La Michezo

Ijumaa, Septemba 20, 2019

Michuano ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 Afrika Mashariki na Kati (Kombe la CECAFA Challenge U20) inaanza rasmi Jumamosi hii ya Septemba 21, 2019 mjini Kampala, Uganda.

Mashindano hayo yanashirikisha mataifa 11 yaliyogaanywa katika makundi matatu.
Mechi ya kufungua dimba ni kati ya Sudan na Djibouti kuanzia mchana saa 14:00hrs(EAT) kabla ya wenyeji Hippos ya Uganda kupambana na Eritrea kuanzia alasiri saa 16:00hrs(EAT).

Mechi hizo za kundi A, zitafanyika Pece War Memorial Stadium huko Gulu kaskazini mwa mji wa Kampala. Uwanja mwengine utakaotumika wa FUFA Technical Centre Njeru ulio mashariki mwa Kampala.

Wenyeji Hippos ya Uganda, wanaofunzwa na kocha Morley Byekwaso, wamepangwa Kundi A pamoja na Sudan, Eritrea, Djibouti wakati Kundi B likiwa na Rising Stars ya Kenya, Ethiopia, Ngorongoro Heroes ya Tanzania na Zanzibar ilhali Burundi, Sudan Kusini na Somalia zimepangwa kwenye Kundi C.

Kwa mujibu wa ratiba ya michuano hiyo, siku ya Jumapili ya Septemba 22, kutachezwa mechi mbili za kundi B, vijana wa kocha Stanley Okumbi Rising Stars ya Kenya wataanza kuvaana na vijana wa Zanzibar kuanzia mchana saa 14:00hrs(EAT) kabla ya Ethiopia kuwakabili Ngorongoro Heroes ya Tanzania, wanaonolewa na Kocha Zubery Katwila, kuanzia alasiri saa 16:00hrs(EAT)

Rising Stars ya Kenya itashuka tena dimbani Septemba 24 kuwavaa Ngorongoro Heroes na kumaliza mechi zake za Kundi B kwa kupambana na Ethiopia huku Ngorongoro Heroes wakimaliza kwa ndugu zao, Zanzibar.

Mechi za hatua ya Robo Fainali zitapigwa Septemba 29, Nusu Fainali Okatoba 2 na Fainali ya michuano ya CECAFA Challenge U20 mwaka 2019 itafanyika Oktoba 5.

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin