Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

FKF NSL: Stima, City Stars, Bidco United zafukusana uongozini

Na Anthony Aroshee

Jumatano, Septemba 25, 2019

Nairobi Stima FC, Nairobi City Stars na Bidco United FC kutoka Thika ndizo zinazoshikilia nafasi tatu-Bora za kwanza katika msimamo wa jedwali ya Supaligi ya Taifa NSL ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Kenya, FKF.

Nairobi Stima FC na Nairobi City Stars wana alama 13 kila mmoja wakiwa kwenye nafasi ya kwanza na pili mtawalia huku Nairobi Stima ikiizidi kete Nairobi City Stars kwa Ubora wa mabao ya kufunga na kufungwa, wote kwa pamoja, wakiwa na alama moja zaidi ya Bidco United FC iliyo ya tatu kwa alama 12.
Timu hizo zilifikisha alama hizo baada ya kushinda mechi za ligi hiyo zilizopigwa siku ya Jumatatu iliyopita.

Nairobi Stima FC ilipata ushindi wa mabao 2-0 nyumbani dhidi ya wenyeji wao timu ya Fortune Sacco FC kwenye Uwanja wa Karuturi, nayo Nairobi City Stars walikuwa ugenini mjini Mombasa na kuwashinda Coast Stima FC mabao 2-1 katika Uwanja wa KPA Sports Club Mbaraki.

Nayo Bidco United FC, ambayo ilikuwa nyumbani, iliicharaza Muranga Seal kwa kuinyeshea mvua ya mabao 5-0 katika mchezo uliofanyika Thika Stadium. Emmanuel Mogaka na Eric Kahunge, walipachika wavuni mabao mawili kila mmoja huku Anthony Simasi akifunga bao moja.

FC Talanta ya Nairobi, ambayo iko katika nafasi ya nne baada ya kufikisha alama 10, waliwachapa wageni wao timu ya Northern Wanderers FC mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Camp Toyoyo.

Wageni ndio waliokuwa wa kwanza kufunga bao la kuongoza kupitia Enock Momanyi dakika ya nane kabla ya FC Talanta kufungwa mabao yake matatu katika kipindi cha pili, yaliyofungwa na washambuliaji Antony Gachiu dakika ya 16, Abdul Wahab dakika ya 26 na Brian Juma katika dakika ya 31.

Hiyo ni mechi ya tano Northern Wanderers FC kupoteza hadi kufikia sasa ikivuta mkia bila alama.
Mount Kenya FC ndio wanaofunga kurasa ya tano-Bora kwenye msimamo wa ligi ya NSL wakiwa na alama 10 katika nafasi ya tano wakiwa wameshindwa na FC Talanta kwa Ubora wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Mount Kenya ilipata ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya wenyeji wao APS Bomet mechi iliyofanyika Kericho Green Stadium.

Ligi hiyo itaendelea tena Jumamosi ijayo ya Septemba 28, 2019.

MATOKEO KAMILI JUMATATU

Kenya Police 2-2 Migori Youth (Karuturi Grd)
Modern Coast Rangers 1-1 Vihiga United (Serani Sports Club)
Northern Wanderers 1-3 FC Talanta (Camp Toyoyo)
Ushuru 1-1 Kibera Black Stars (Ruaraka Grd.)
APS Bomet 0-2 Mount Kenya (Kericho Green Stadium)
Murang’a Seal 0-5 Bidco United (Thika Stadium)
St Joseph’s Youth 1-2 Vihiga Bullets (Afraha Stadium)
Administration Police 2-0 Shabana (Camp Toyoyo)
Coast Stima 1-2 Nairobi City Stars (Mbaraki Sports Club)
Nairobi Stima 2-0 Fortune Sacco (Karuturi Grd)

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin