Yanayojiri

Afcon Qualifier 2021:Kundi A: Namibia, Mali, Guinea, Chad. Kundi B: Uganda, Sudan Kusini, Malawi, Burkina Faso. Kundi C: Sudan, Ghana, Afrika Kusini, Sao Tome na Principe. Kundi D: Gambia, Gabon, DR Congo, Angola. Kundi E: Morocco, Mauritania, Jamhuri ya Kati, Burundi. Kundi F: Rwanda, Msumbiji, Cape Verde, Cameroon (mwenyeji). Kundi G: Togo, Kenya, Misri, Comoros. Kundi H: Zimbabwe, Zambia, Botswana, Algeria (Watetezi). Kundi I: Senegal, Guinea-Bissau, eSwatini (zamani Swaziland), Congo Brazzaville. Kundi J: Tunisia, Tanzania, Libya, Equatorial Guinea. Kundi K: Niger, Madagascar, Ivory Coast, Ethiopia. Kundi L: Sierra Leone, Nigeria, Lesotho, Benin.Afcon Qualifier 2021:Jumatano, Novemba 13, 2019. Namibia v Chad, Burkina Faso v Uganda, Malawi v Sudan Kusini, Sudan v Sao Tome na Principe, Angola v Gambia, Jamhuri ya Kati v Burundi, Cameroon v Cape Verde, Senegal v Congo Brazaville, Guinea-Bissau v E-eSwatini, Nigeria v Benin, Sierra Leone v Lesotho.. Afcon Qualifier 2021:Alhamisi, Novemba 14, 2019. Mali v Guinea, Ghana v Afrika Kusini, DR Congo, Msumbiji v Rwanda, Misri v Kenya, Togo v Comoros, Algeria v Zambia.Afcon Qualifier 2021:Ijumaa, Novemba 15, 2019. Morocco v Mauritania, Zimbabwe v Botswana, Tunisia v Libya, Tanzania v Equatorial Guinea.Afcon Qualifier 2021:Jumamosi, Novemba 16, 2019. Ivory Coast v Niger, Madagascar v Ethiopia.Afcon Qualifier 2021:Jumapili, Novemba 17, 2019. Guinea v Namibia, Chad v Mali, Uganda v Malawi, Sudan Kusini v Burkina Faso, Afrika Kusini v Sudan. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

FKF Western Branch League 2019/2020: Msimu mpya unaanza Jumamosi hii

Na Anthony Aroshee

Alhamisi, Septemba 26, 2019

Mshikemshike wa msimu mpya 2019/2020 wa Ligi ya Shirikisho la Kabumbu nchini Kenya FKF Tawi la Magharibi, unaanza rasmi mwishoni mwa juma hili kwa mitanange 14 kwenye viwanja tofauti ukishirikisha timu 26 zilizogaanywa katika Kanda tatu.

Msimu huo mpya unaanza Jumamosi hii ya Septemba 28, 2019.

Kanda A itakuwa na timu nane za kutoka Kaunti ya Vihiga ambazo ni Luanda Sports FC, 11 Jaws FC, Hearts Academy FC, Maseno United FC, Rangers FC, Chandumba FC, Bugembe FC na Shooting Stars FC.

Kanda B imeorodhesha timu 10 za Kaunti ya Kakamega ambazo ni One Acre Fund FC, Lugusi Boys FC, Kabras United FC, The Scorpions FC, MYSA FC, The Rock Saints FC, The Sleemaz FC, Munganga FC na Eshitari FC.

Nayo Kanda C inajumuisha timu nane za kutoka Kaunti ya Busia ambazo ni Mayenje Santos FC, St.Anthony Okatekok FC, Mungatsi FC, Marenga Warriors FC, Busia Sugar FC, Busia Allstars FC, New WECO FC na Dragons FC.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Katibu Mkuu ambaye pia ni Afisa Mkuu Mtendaji CEO wa Shirikisho hilo la Soka FKF Tawi la Magharibi Kevin Mwangu, Jumamosi hii kunachezwa mechi saba ambazo zote zitaanza kwa pamoja mchana saa 13:00hrs(EAT).

Maseno United FC wanaanzia nyumbani kwa kuwaalika wageni Shooting Stars FC kwenye Uwanja wa Maseno VCT huku 11 Jaws FC wakifungua msimu mpya kwa kucheza ugenini dhidi ya wenyeji wao Bugembe FC, mechi itakayogaragazwa Mumboha Stadium.

Kabras United FC itawaalika vijana wa Lugusi Boys FC kwenye Uwanja wa shule ya upili ya Shamoni nao Ng’e The Scorpions FC watakuwa wenyeji wa Munganga FC katika Uwanja wa shule ya Musingu huku One Acre Fund FC wakikaribishwa ugenini na Rosterman United FC kwenye Uwanja wa shule ya upili ya Rosterman.

Mayenje Santos FC watashuka dimbani wakiwa wenyeji dhidi ya New WECO FC kwenye Uwanja wa shule ya msingi ya Mayenje wakati Marenga Warriors FC watamenyana na Busia Allstars FC katika mechi itakayochezwa Siagonjo Grounds.

Na hapo Jumapili Septemba 29, pia kumepangwa kuchezwa mechi nyingine saba ambazo pia zitaanza mchana saa 13:00hrs(EAT). Hearts Academy FC watapambana na wageni Chandumba FC kwenye Uwanja wa shule ya upili ya Kegoya, Kabras Allstars FC watakuwa ugenini kuvaana na weneyji wao The Sleemaz FC katika Uwanja wa Muslim Boys.

The Rock Saints FC watawakaribisha Lubinu Rangers FC kwenye Uwanja wa St.Peters Boys wakati vijana wa Eshitari FC wataonana na MYSA FC kwenye Uwanja wa shule ya upili ya Eshitari huku Mungatsi FC wakichuana na St.Anthony Okatekok FC kwenye Uwanja wa shule ya msingi ya Mungatsi.

Busia Sugar FC wataanza msimu mpya ugenini kwa kukwatuana na wenyeji wao timu ya Dragons FC kwenye Uwanja wa shule ya msingi ya Nyakwaka kabla ya Luanda Sports FC kuwaalika vijana wa Rangers FC mechi ambayo itafanyika Mumboha Stadium kuanzia alasiri saa 15:15hrs(EAT)

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin