Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

Chapa Dimba Na Safaricom kuanza Malindi wikendi hii 

Na Anthony Aroshee

Ijumaa, Septemba 27, 2019

Michuano ya Soka makala ya tatu ya kuvumbua vipaji miongoni mwa vijana ya kuwania taji la Chapa Dimba na Safaricom 2019 katika tawi la Pwani Kaskazini ya Shirikisho la Kandanda nchini Kenya FKF, inaanza Jumamosi hii ya Septemba 28,2019 ikishirikisha timu 16.

Kinyang’anyiro hicho kinaandaliwa katika tawi dogo la FKF la Malindi. Kati ya timu hizo, timu tatu ni za Wasichana na timu nyingine 13 ni za Wavulana.
Timu za Wavulana zimepangwa kwenye makundi A hadi D ilhali kundi moja lina timu za Wasichana ambapo mechi zao zitaanza kuchezwa Jumamosi ya Oktoba 5, 2019.

Mechi za hatua ya makundi ya michuano hiyo ya Chapa Dimba na Safaricom zitachezwa katika viwanja vya shule ya msingi ya Malindi Central na Holy Ghost Memorial H.G.M pamoja na viwanja vya St.Andrew, Furunzi na Gongoni.

Mechi za kufungua dimba Jumamosi hii za Kundi A, ambazo zitasakatwa kwenye Uwanja wa St.Andrew, timu ya Kisumu Ndogo United FC wataanza kukwatuana na Malindi Cluster FC kabla ya Malindi Cluster FC kushuka tena dimbani kucheza mechi yao ya mwisho dhidi ya Mtangani United FC. Mechi ya mwisho katika kundi hilo itakuwa kati ya Mtangani United FC na Kisumu Ndogo United FC.

Na kwenye Uwanja wa shule ya msingi ya Malindi Central kutakapopigwa mechi za Kundi B, Yanga FC dhidi ya Barani Ballers FC kisha mchezo wa pili uwakutanishe Barani Ballers FC na Inter-Dabaso FC kabla ya Yanga kumalizana na Inter-Dabaso FC katika mechi ya tatu na ya mwisho kwenye kundi hilo.

Na siku ya Jumapili ya Septemba 29, Amazing Grace watamenyana na Malindi Youth FC katika mpambano wa Kundi C kwenye Uwanja wa Furunzi huku Muyeye Secondary School FC kukipiga dhidi ya Amazing Grace. Mechi ya mwisho ni baina ya Malindi Youth FC na Amazing Grace FC.

Katika Kundi D kutachezwa mechi mbili tu ambazo zitakuwa za mtoano. Maweni United FC wataonana na Real Malindi FC kwenye Uwanja wa shule ya msingi ya Holy Ghost Memorial H.G.M wakati FC Black Panther watapepetana na Imarika Sacco FC Uwanjani Gongoni.

Mechi hizo zitaanza asubuhi saa 09:00hrs(EAT).

Kila kundi litatoa timu mbili Bora ambazo zitasonga mbele katika hatua nyingine.
Michuano hiyo ya kuvumbua vipaji ya Chapa Dimba na Safaricom inashirikisha Soka ya Wasichana na Wavulana wenye umri kati ya miaka 16 na 20 ukiwa ni mkakati wa kukuza soka mashinani, yanayoendeshwa kwa ushirikiano wa Shirikisho la Soka nchini Kenya FKF.

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin