Yanayojiri

Afcon Qualifier 2021:Kundi A: Namibia, Mali, Guinea, Chad. Kundi B: Uganda, Sudan Kusini, Malawi, Burkina Faso. Kundi C: Sudan, Ghana, Afrika Kusini, Sao Tome na Principe. Kundi D: Gambia, Gabon, DR Congo, Angola. Kundi E: Morocco, Mauritania, Jamhuri ya Kati, Burundi. Kundi F: Rwanda, Msumbiji, Cape Verde, Cameroon (mwenyeji). Kundi G: Togo, Kenya, Misri, Comoros. Kundi H: Zimbabwe, Zambia, Botswana, Algeria (Watetezi). Kundi I: Senegal, Guinea-Bissau, eSwatini (zamani Swaziland), Congo Brazzaville. Kundi J: Tunisia, Tanzania, Libya, Equatorial Guinea. Kundi K: Niger, Madagascar, Ivory Coast, Ethiopia. Kundi L: Sierra Leone, Nigeria, Lesotho, Benin.Afcon Qualifier 2021:Jumatano, Novemba 13, 2019. Namibia v Chad, Burkina Faso v Uganda, Malawi v Sudan Kusini, Sudan v Sao Tome na Principe, Angola v Gambia, Jamhuri ya Kati v Burundi, Cameroon v Cape Verde, Senegal v Congo Brazaville, Guinea-Bissau v E-eSwatini, Nigeria v Benin, Sierra Leone v Lesotho.. Afcon Qualifier 2021:Alhamisi, Novemba 14, 2019. Mali v Guinea, Ghana v Afrika Kusini, DR Congo, Msumbiji v Rwanda, Misri v Kenya, Togo v Comoros, Algeria v Zambia.Afcon Qualifier 2021:Ijumaa, Novemba 15, 2019. Morocco v Mauritania, Zimbabwe v Botswana, Tunisia v Libya, Tanzania v Equatorial Guinea.Afcon Qualifier 2021:Jumamosi, Novemba 16, 2019. Ivory Coast v Niger, Madagascar v Ethiopia.Afcon Qualifier 2021:Jumapili, Novemba 17, 2019. Guinea v Namibia, Chad v Mali, Uganda v Malawi, Sudan Kusini v Burkina Faso, Afrika Kusini v Sudan. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

Wananyuki na Mvita Young Stars kuvaana fainali ya Mvita Pre-Season Soccer

Na Anthony Aroshee

Jumamosi, Septemba 28, 2019

Klabu za Wananyuki FC na Mvita Young Stars FC watamenyana katika kipute cha fainali ya kuwania taji la michuano ya Mvita Pre-Season Soccer kitakachopigwa alasiri ya Jumamosi hii ya Septemba 28, 2019 kwenye Uwanja wa MTTI(Bomani) huko Tononoka mjini Mombasa nchini Kenya.

Mpambano huo utaanza alasiri hii saa 16:00hrs(EAT) kwenye Uga huo ulio katika eneo bunge la Mvita.

Kutakuwa na zawadi nyingi zitakazotolewa kwa washindi kama vile vikombe, medali, jezi, mipira na pesa taslimu.
Mtanange huo unatarajiwa kuhudhuriwa na mbunge wa eneo la Mvita Abdulswamad Shariff Nassir, Wawakilishi wa wadi za Tononoka na Majengo katika bunge la Kaunti ya Mombasa MCA Ali Shariff ‘Kipenzi Cha Watu’ na Ahmed Nyundo, miongoni mwa wageni wengine.

Timu hizo Wananyuki FC na Mvita Young Stars FC zilifanikiwa kutinga fainali baada ya kuibuka videdea katika mechi za hatua ya nusu fainali huku Wananyuki FC wakiwashinda vijana wa Congo Boys FC baada ya kuwafunga mabao 2-1.
Nao Mvita Young Stars FC waliwashinda KCN Poly mabao 5-4 kupitia mikwaju ya matuta baada ya timu hizo kutoka sare ya 0-0 katika muda wa dakika 90 katika mchezo mwengine wa nusu fainali.

Na katika vipute vya robo fainali, Wananyuki FC walipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Dragon FC wakati Mvita Young Stars FC wakiwafunga Boca Juniors FC mabao 3-2.
Mechi nyingine za robo fainali, Congo Boys FC waliwavumua Veterans FC mabao 3-0 huku KCN Poly wakiwalaza Momabasa Hamlets FC mabao 3-1.

Katika mechi za hatua ya makundi, Wananyuki FC walikuwa kwenye Kundi C na kumaliza kileleni kwa kujizolea jumla ya alama sita ambapo walianza vibaya kwa kupata kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Boca Juniors FC.
Wananyuki FC wakawavuruga vibaya Tononoka Sports FC kwa kuwadunga mabao 4-1 huku wakifunga kazi katika kundi hilo kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Kilifi Youth.

Nao Mvita Young Stars FC waliorodheshwa katika Kundi D na kumaliza vigogo baada ya kuambulia alama tisa.
Walianza kibabe kwa kuwanyeshea Bantu Warriors FC mvua ya mabao 6-1 kisha wakaendeleza tena ubabe wao kwa Dragon FC walipowapiga ‘mukono’ mabao 5-1 kabla ya kumaliza vyema kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya vijana wa Spartak Moons FC.

Michuano hiyo imeandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Kenya FKF tawi dogo la Mombasa, chini ya mwenyekiti wake Goshi Juma, kwa madhumuni ya kuzipa timu nafasi ya kujiandaa mapema kabla ya msimu mpya 2019/2020 wa ligi zinazosimamiwa na FKF Sub Branch kuanza baadae mwaka huu.

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin