Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

Wananyuki watwaa Ubingwa wa Mvita Pre-Season Soccer Tournament

Na Anthony Aroshee

Jumatano, Oktoba 2, 2019

Timu ya Wananyuki FC walifanikiwa kuwashinda Mvita Young Stars FC katika kipute cha fainali na kutwaa Ubingwa wa michuano ya kuwania taji la Mvita Pre-Season Soccer iliyoandaliwa katika eneo bunge la Mvita Kaunti ya Mombasa nchini Kenya.

Wananyuki FC walipata ushindi huo wa mabao 4-3 kupitia mikwaju ya matuta baada ya timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2 katika muda wa kawaida wa dakika 90 katika fainali iliyopepetwa Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Mombasa Technical Training Institute MTTI(Bomani) ulioko eneo la Tononoka.

Vijana wa Wananyuki FC walijipatia mabao yao yaliyotumbukizwa kimyani na Abdallah Ali na Brian Moraya nayo timu ya Mvita Young Stars FC walifunga mabao yaliyomiminwa wavuni na Abdulmajid Chibaa na Abdulrahman Mohamed.

Katika upigaji wa mikwaju ya penalti, Wananyuki FC walifunga matuta yao kupitia Brian Moraya, Ian Bilal, Ali Juma na Abdul Jabar huku Ayub Khalid na Juma Ali wakishindwa kufunga penalti zao. Mvita Young Stars FC walifunga matuta yao kupitia za Athman Twaha, Abdulrahman Mohamed na Said Maxwell nao Ali Makame, Ahmed Abubakar na Abdulmajid Chibaa walipoteza mikwaju yao ya penalti.

Wananyuki FC na Mvita Young Stars FC walikutana katika fainali hiyo baada ya kushindi mechi za hatua ya nusu fainali.
Wananyuki FC waliwafunga Congo Boys FC mabao 2-1 ilhali Mvita Young Stars FC walitinga fainali kwa kupata ushindi dhidi ya KCN Poly FC wa mabao 5-4 kwa njia ya upigaji wa mikwaju ya matuta baada ya mechi hiyo kuishia sare ya 0-0 kwenye muda wa kawaida wa dakika 90.

Na kwenye mechi za robo fainali, Wananyuki FC walipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Dragon FC wakati Mvita Young Stars FC waliwafunga Boca Juniors FC mabao 3-2.

Katika mechi za hatua ya makundi, Wananyuki FC walikuwa kwenye Kundi C na kumaliza kileleni kwa kujizolea jumla ya alama sita ambapo walianza vibaya kwa kupata kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Boca Juniors FC.
Wananyuki FC wakawavuruga vibaya Tononoka Sports FC kwa kuwadunga mabao 4-1 huku wakifunga kazi katika kundi hilo kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Kilifi Youth.

Nao Mvita Young Stars FC waliorodheshwa katika Kundi D na kumaliza vigogo baada ya kuambulia alama tisa.
Walianza kibabe kwa kuwanyeshea Bantu Warriors FC mvua ya mabao 6-1 kisha wakaendeleza tena ubabe wao kwa Dragon FC walipowapiga ‘mukono’ mabao 5-1 kabla ya kumaliza vyema kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya vijana wa Spartak Moons FC.

Michuano hiyo iliandaliwa na Shirikisho la Soka nchini FKF tawi dogo la Mombasa, chini ya mwenyekiti wake Goshi Juma, kwa madhumuni ya kuzipa timu nafasi ya kujiandaa mapema kabla ya msimu mpya 2019/2020 wa ligi zinazosimamiwa na Shirikisho hilo kuanza mwishoni mwa wikendi hii.

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin