Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

Soweto wababe wa Mvita Pre-Season Soccer Tournament

Na Anthony Aroshee

Jumatano, Oktoba 2, 2019

Klabu ya Soweto FC ilitangazwa bingwa na kunyanyua kombe la michuano ya kuwania taji ya Mvita Pre-Season Soccer kwa kuishinda timu ya Magongo Rangers FC katika mtanange wa fainali iliyogaragazwa Jumapili iliyopita kwenye Uwanja wa Bomu huko Changamwe katika Kaunti ya Mombasa.

Soweto FC iliishinda Magongo Rangers mabao 4-3 katika upigaji wa mikwaju ya matuta baada ya vijana hao wa timu hizo mbili kumaliza fainali hiyo bila mshindi kupatikana kwa kutoka sare ya 0-0 baada ya muda wa kawaida wa dakika 90 kumalizika.

Katika upigaji wa maguu 12 ya mtu mzima, Soweto FC ilifunga matuta yao kupitia Juma Maulidi, Yusuf Mohamed, Mohamed Mwinyi na Juma Mwinyi huku tuta za Rama Rajab, Shaaban Rajab zikishindwa kuingia langoni.

Matuta ya Magongo Rangers FC yalifungwa na Said Jule, Mohammed Badidi na Abuu Simao nao Kassim Hamza, Davies Olouch na Suleiman Daco walishindwa kufunga matuta yao.

Klabu ya Soweto FC, inayonolewa na kocha Abdulrahman Mwinyi, ilifuzu fainali kwa kuinyuka Ashton Rangers FC bao 1-0 katika mchezo wa nusu fainali wakati nayo Magongo Rangers FC, pia ilipata ushindi kama huo dhidi ya timu ya Coolchester FC katika mechi nyingine ya nusu fainali.

Katika mechi za hatua ya makundi, Soweto FC iliwazaba Umba Sports Club bao 1-0 kisha ikawachapa Wayani United mabao 4-0 kabla ya kuwadunga Hidden Talent FC mabao 4-2.

Nayo Magongo Rangers FC ilipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Nyota FC na Chaani Youth FC kabla ya kuwalemea Wazee Health FC kwa kuitandika mabao 5-0.

Michuano hiyo iliandaliwa na Shirikisho la Soka nchini FKF tawi dogo la Mombasa, chini ya mwenyekiti wake Goshi Juma, kwa madhumuni ya kuzipa timu nafasi ya kujiandaa mapema kabla ya msimu mpya 2019/2020 wa ligi zinazosimamiwa na Shirikisho hilo kuanza mwishoni mwa wikendi hii.

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin