Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

CECAFA Challenge U20: Kenya kuwakabili Tanzania fainali

Na Dawati La Michezo

Ijumaa, Oktoba 4, 2019

Rising Stars ya Kenya na Ngorongoro Heroes ya Tanzania watapambana katika kipute cha fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 20, CECAFA Challenge U-20 ya mwaka huu 2019 inayofanyika nchini Uganda.

Patashika hiyo itachezwa Jumamosi hii ya Oktoba 5, 2019 kwenye Uwanja wa Kituo cha Ufundi cha Shirikisho la Soka Uganda (FUFA). Ikumbukwe Kenya na Tanzania, ambazo zinanolewa na makocha wazawa, zimetoka katika Kundi B na mechi baina yao ilimalizika kwa sare ya kufungana mabao 2-2.

Tanzania, ambayo inafunzwa na Kocha wa klabu ya Mtibwa Sugar Zubery Katwila, iliingia fainali baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Sudan katika mechi ya kwanza ya nusu fainali iliyochezwa kwenye Uwanja wa Kituo cha Ufundi cha Shirikisho la Soka Uganda (FUFA).
Mabao ya Tanzania Bara yalifungwa na Israel Patrick Mwenda dakika ya 36 na Kelvin Pius John dakika 45 huku bao la Sudan likifungwa na Mohamed Abbas Namir dakika ya 56.

Na katika mechi ya pili ya nusu fainali iliyochezwa kwenye Uwanja wa Guru huko Njeru, mlinzi wa Eritrea Yosief Mebrahtu, alijifunga langoni kwake dakika ya 84 bao lililoipa vijana wa Kenya, wanaofunzwa na kocha Stanley Okumbi, ushindi wa bao 1-0 na kutinga fainali.

Sudan na Eritrea watachuana katika mechi ya kumtafuta mshinde wa tatu.

Katika mechi za hatua ya robo fainali, ‘Ngorongoro Heroes iliwazaba wenyeji Hippos ya Uganda, wanaofunzwa na kocha Morley Byekwaso, mabao 4-2 wakati Rising Stars ya Kenya waliwafunga Burundi mabao 2-1.

Robo Fainali nyingine Sudan iliichuna Sudan Kusini bao 1-0 na Eritrea wakawafanya vibaya Zanzibar kwa kuwadunga mabao 5-0.
Michuano hiyo inashirikisha mataifa 11 ambayo ni Sudan, Eritrea, Djibouti, Kenya, Ethiopia, Tanzania Bara, Zanzibar, Burundi, Sudan Kusini, Somalia na wenyeji Uganda.

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin