Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

Msimu mpya FKF Mombasa Premier League unaanza

Na Anthony Aroshee

Ijumaa, Oktoba 4, 2019

Magongo Rangers FC na Bandari Youth FC watapambana katika ngarambe ya kufungua dimba la pazia ya msimu mpya 2019/2020 wa Mombasa Premier League ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Kenya FKF tawi dogo la Mombasa.

Patashika hiyo itapigwa kwenye Uwanja wa Bomu huko Changamwe kuanzia alasiri saa 15:30hrs(EAT).

Msimu huu mpya wa ligi hiyo, unashirikisha jumla ya timu 18 huku timu tatu Change Youth FC, KCN Poly FC na Tononoka Sports FC ndizo zilizopandishwa Daraja kutoka ligi Daraja la Kwanza msimu uliopita.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Shirikisho hilo la Kabumbu la FKF tawi dogo la Mombasa, chini ya mwenyekiti wake Goshi Alliy Juma, ligi hiyo itaingia siku yake ya pili Jumapili hii ya Oktoba 6, 2019 kwa kuchezwa mechi nyingine nane, ambazo pia zitaanza alasiri saa 15:30hrs(EAT) kwenye viwanja mbali mbali.

Klabu ya Westham FC wanaanza msimu mpya kwa kuwaalika wageni Junda Strickers FC kutoka Mishomoroni katika mechi ambayo itafanyika kwenye Uwanja wa Ziwani Lasco wakati Crossroads FC kutoka maeneo ya Nyali, watafunga safari hadi Mikindani eneo bunge la Jomvu kuwakabili wenyeji wao Golden Boys FC kwenye Uwanja wa shule ya msingi ya Kwa Shee.

Nao Wanderers FC kutoka Mvita wanafungua msimu mpya kwa kuwakaribisha Nyali Youth FC katika Uwanja wa Tononoka ilhali Bamburi United FC watavuka kivuko cha Likoni kuwafuata wenyeji wao vijana wa Zaragoza FC mechi ambayo imepangwa kupepetwa Masoud Mwahima Stadium.

Umba Sports Club FC kutoka Magongo eneo bunge la Changamwe wanaanzia ugenini kwani wao pia watafunga safari na kuvuka daraja la nyali kwenda kuwavaa wenyeji wao Mantubila FC kwenye Uwanja wa Mantubila huko Shanzu eneo bunge la Kisauni.

Change Youth FC kutoka Likoni wako nyumbani dhidi ya wageni Tononoka Sports FC kwenye Uwanja wa Panama huku KCN Poly FC wakiwa wenyeji wa Soweto FC katika Uwanja wa Mombasa Technical Training Institute MTTI(Bomani) ulioko eneo la Tononoka.

Annex FC kutoka Majaoni wanaanzia ugenini dhidi ya vijana wa Coolchester FC katika mchezo utakaogaragazwa kwenye Uwanja wa Wayani Muembeni.

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin