Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

FKF Mombasa Sub Branch kutunuku mabingwa wa Ligi

Na Anthony Aroshee

Ijumaa, Oktoba 4, 2019

Shirikisho la Kabumbu nchini Kenya FKF tawi dogo la Mombasa, Jumamosi hii ya Oktoba 5, 2019 litatunuku kwa kutoa zawadi kwa timu zilizofanikiwa kunyanyua Ubingwa wa ligi tano za Shirikisho hilo zilizofanyika msimu uliopita.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa Shirikisho hilo Goshi Alliy Juma, hafla hiyo imeandaliwa kufanyika mwendo wa alasiri kwenye Uwanja wa Bomu huko Changamwe muda mfupi kabla ya mtanange wa kufungua msimu mpya 2019/2020 wa Mombasa Premier League ya Shirikisho hilo kati ya Magongo Rangers FC na Bandari Youth FC kuanza katika Uwanja huo.

Miongoni mwa wageni waalikwa katika hafla hiyo, ni Seneta wa Kaunti ya Mombasa Mohamed Faki pamoja na Mwakilishi wa Wadi ya Portreitz huko Changamwe katika bunge la Kaunti ya Mombasa ambaye pia ni naibu wa Spika wa bunge hilo, MCA Fadhili Mwalimu.

Changamwe FC ndio iliyotwaa Ubingwa wa FKF Mombasa Premier League nayo Change Youth FC ilishinda Ubingwa wa Ligi Daraja la Kwanza wakati GuardForce Sakawa FC iliibuka kidedea kwa kutangazwa bingwa wa Ligi Daraja la pili.

Timu ya Okoa Ladies FC waliibuka mabingwa wa Ligi ya Wanawake huku Fetuwe Wazee FC wakimaliza kileleni kwa kushinda Ubingwa wa ligi ya ‘Wakongwe’ ya Veterans League.

Baada ya msimu huu mpya 2019/2020 wa FKF Mombasa Premier League kuanza Jumamosi hii, ligi hiyo itaendelea tena siku ya Jumapili hii ya Oktoba 6, 2019 kukichezwa jumla ya mechi nane, zote zikianza kwa pamoja alasiri saa 15:30hrs(EAT) kwenye viwanja mbali mbali.

Westham FC ni wenyeji wa Junda Strickers FC kwenye Uwanja wa Ziwani Lasco, Crossroads FC watakuwa ugenini dhidi ya Golden Boys FC katika Uwanja wa shule ya msingi ya Kwa Shee.

Nao Wanderers FC watakaribisha Nyali Youth FC kwenye Uwanja wa Tononoka nao Bamburi United FC wacheza ugenini dhidi ya Zaragoza FC mechi itakayosakatwa Masoud Mwahima Stadium.

Umba Sports Club FC watakuwa ugenini kuwavaa wenyeji wao Mantubila FC Uwanjani Mantubila, Change Youth FC watawaalika Tononoka Sports FC kwenye Uwanja wa Panama. KCN Poly FC ni wenyeji wa Soweto FC kwenye Uwanja wa Mombasa Technical Training Institute MTTI(Bomani) ulioko eneo la Tononoka.

Annex FC wanaanzia ugenini kwa kukabana koo na Coolchester FC kwenye Uwanja wa Wayani Muembeni.

Ligi hiyo inashirikisha timu 18 huku timu tatu Change Youth FC, KCN Poly FC na Tononoka Sports FC ndizo zilizopandishwa Daraja kutoka ligi Daraja la Kwanza msimu uliopita.

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin