Yanayojiri

SOKA:Francesco Totti aachana na AS Roma kama mkurugenzi wa ufundi.CECAFA:Simba SC na Yanga SC zajiondoa kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.CECAFA:TP Mazembe, DC Motema Pembe, AS Vita Club na Zesco United kushiriki Kagame Cup 2019 nchini Rwanda.AFCON 2019:Kundi A DR Congo,Misri, Uganda, Zimbabwe. Kundi B Burundi, Guinea, Madagascar, Nigeria. Kundi C Algeria, Kenya, Senegal, Tanzania. Kundi D Ivory Coast, Morocco, Namibia, Afrika Kusini. Kundi E Angola, Mali, Mauritania, Tunisia. Kundi F Benin, Cameroon, Ghana, Guinea-Bissau. CECAFA: Tanzania mwenyeji wa CECAFA Senior Challenge Cup 2019 Wanawake.CECAFA: Kenya mwenyeji wa CECAFA 2019 U-17 Wanawake. CECAFA: Uganda kuandaa CECAFA Senior Challenge Cup 2019.CECAFA::Eritrea kuandaa CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-17.CECAFA:Rwanda mwenyeji CECAFA Kagame Cup 2019.CECAFA:Uganda mwenyeji CECAFA Challenge Cup 2019 ya U-20 Wanawake.

‘Kufa na kupona’ kati ya Harambee Starlets na Black Queens ndani ya Kasarani

Na Dawati La Michezo

Jumanne, Oktoba 8, 2019

Timu ya taifa ya Kenya ya Wanawake ya Harambee Starlets wanawaalika Black Queens ya Ghana katika kipute cha mkondo wa pili kuwania tiketi ya kufuzu kushiriki kwenye Mashindano ya Olimpiki ya majira ya kiangazi ya mwaka 2020 yatakayoandaliwa mwaka 2020 nchini Japan.

Mpambano huo wa ‘Kufa mtu’, kwa upande wa timu zote mbili, unapepetwa Jumanne hii ya Oktoba 8, 2019 kuanzia alasiri hii saa 16:00hrs(EAT) kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Michezo wa Moi Kasarani jijini Nairobi.

Kiingilio kutazama mechi hiyo ni bure.

Katika mechi ya mkondo wa kwanza uliofanyika Ijumaa iliyopita mjini Accra, Harambee Starlets wanaofunzwa na kocha David Ouma, waliwalazimisha warembo wa kocha Mercy Tagoe Quarcoo Black Queens kutoka nao sare ya 0-0.

Timu itakayofanikiwa kusonga mbele, itakutana na Botswana ama Copper Queens ya Zambia. Timu hizo pia zinacheza mechi nyingine ya mkondo wa pili Jumanne hii mjini Francistown ambapo Botswana iko nyumbani dhidi ya Zambia.

Zambia iliizaba Botswana bao 1-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliochezwa Jumatano iliyopita mjini Lusaka.

Chapa Barua pepe

Share

Dula - Bila wewe

Kocha wa Bandari FC Twahir Muhidin